Skip to main content

Full text of "Elisi katika nchi ya ajabu"

See other formats

ELISI 
KATIKA NCHI YA A JABU ELISI KATIKA NCHI YA AJABU ELISI KATIKA 
NCHI YA AelABU LEWIS CARROLL IMBTAFSIRIWA NA 
St Lo DE MALET [Alice in Wonderland : Swahili] LONDON 

THE SHELDON PRESS 

HOLY TRINITY CHURCH, MARYLEBONE ROAD, N.W.l. 

1967 

1 First published, 1940 MADE IN OREAT BRITAIN YALIYOMO 8URA 

I. Pango la Sunguba 
n. Ktdtmbwi cha Maghozi 
ni. Shindano la Kaka 
rv. Nyumba ya Stjnguba 
V. Mashaubi ya Mdudu 
VI. Ngubuwb na PnjpiLi 
VII. Kabamu ya Wbnyb Wazimu 
VIII. Machbzo ya Malkia - 
IX. Hadithi ya Kasa 
X. Ngoma ya Kamba 
XI. Mwizi WA Maandazi - 

Xn. USHAHTDI WA EUSI UKURASA 

- 11 

- 19 

- 28 

- 34 

- 44 
56 

- 66 

- 75 

- 86 

- 94 

- 101 

- 108 vu W ..Y Zamani sana Mzungu mmoja 
Aliyependwa na watoto, 
Aliwahadithia kwa umoja 
Habari tamu sana za ndoto. 

Na mimi basi ninapenda 
Watoto Waafrika pia, 
Nimefikiri watapenda sana 
Kwa lugha yao nzuri kusikia 

Habari za mtoto yule 
Katika Nchi ya Ajabu. 
Tafsiri yake naam ni kazi kubwa 
Furaha yao kwangu ni thawabu. 

Njoni watoto na kaeni, 
Tutafurahi sana sisi ! 
SikiUzeni nitakaposoma 
Maneno na matendo ya Elisi. 

Ingawa mimi ni Mzungu 
Mniridhie; si mgeni, 
Mna bahati nami bila shaka. 
Sikihzeni sana, nyamazeni. 

E. V. St. L. C.-D. IX MsmB ' 
SURA I 

PANGO LA SUNGURA 

Hapo kale palikuwa na mtoto mwanamke, jina 
lake Elisi. Wakati wa mwanzo wa hadithi hii 
Elisi alikuwa amekaa pamoja na dada yake 
katika kivuli cha mwembe; mara kwa mara 
alikuwa akitazama kitabu alichokuwa akisoma 
dada yake, lakini kilikuwa kitabu kisicho picha ; 
Elisi akasema moyoni mwake, " Kitabu bila 
sanamu hakina faida " akapiga mwayo akanena 
" Nataka niondoke nikachume maua, lakini 
nimechoka kabisa " ! 

Hapo yule EUsi alishtuka kumwona sungura 
mweupe mwenye macho mekundu aliyekuwa 

11 12 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

akikimbia; Elisi hakustaajabu hata alipomsikia 
yule sungura akisema, " Ole wangu, ole wangu ! 
Nitachelewa kabisa." 

(Halafu alikumbuka ya kwamba sungura 
hawasemi, lakini wakati wa hadithi hii haku- 
shangaa.) 

Sungura alitoa saa mfukoni mwake; mara 
Elisi akaondoka akasema " Lo ! sungura ana 
kanzu na mfuko na saa ! Naam hii ni ajabu 
kubwa !" Akapiga mbio, akamfuata shambani, 
na kwa bahati hakumpotea bali alimwona 
akiingia pangoni mwake. 

Elisi hakukaa kufikiri bali akaendelea ku- 
mfuata sungura. Pango liliendelea moja kwa 
moja kwa mwendo wa dakika kumi, kisha njia 
ikatelemka kwa ghafula kama inayoingia kisi- 
mani, na kwa sababu ya giza lililokuwako Elisi 
hakuliona Hle shimo, akatumbukia ; lakini haku- 
lia wala hakuogopa kwa kuwa hakuanguka 
kama jiwe, lakini alitelemka kama kwamba 
alikuwa akiruka hewani, alikuwa akianguka 
pole pole. 

Kwanza Elisi aUjaribu kutazama chini, lakini 
hakuona kitu ila giza tupu, kisha akatazama 
kuta za kisima, na kumbe zilikuwa na makabati 
mengi na vibao vya kuwekea vitabu; huko na 
huko zimetundikwa ramani na sanamu. Katika 
kibao kimoja akaona chupa nyingi sana, aka- 
twaa moja akasoma katika cheti chake " Ma- 
tunda ya Machungwa." Halafu aliogopa kuia- PANGO LA SUNGIJRA 13 

ngusha akasema " Labda pana watu chini, 
nitawadhuru nikiiangusha chupa hii." Lakini 
alijitahidi akairudisha katika kibao kingine. 

EHsi aliwaza, akasema moyoni " Basi, baada 
ya kuanguka namna hii sitaogopa tena kua- 
nguka, hata nikitoka juu ya dari ya nyumba, 
sitalia hata kidogo, jamaa zangu watafurahi 
na kufikiri kuwa mimi ni mtoto hodari sana !" 

Akatelemka ! Akatelemka ! Akatelemka ! 
Akasema " Bila shaka nimetelemka maili nyi- 
ngi sana, labda chini ya kisima hiki ni kati kati 
kabisa ya dunia ! Au labda hakuna mwisho, 
na kisima hiki kitatokea upande wa pili wa 
dunia; je, watu wa upande huo wanafanana na 
nini ? Nikifika huko nitawasujudia, nitawa- 
uliza habari za nchi yao." Ehsi akakumbuka 
ya kwamba Mwahmu wa chuoni alipata kufu- 
ndisha ya kuwa nchi ya Amerika iko upande 
wa pili wa dunia, akasema " Labda nakwenda 
Amerika !" 

Akashuka ! Akashuka ! Akashuka ! Elisi 
akaanza tena kujizungumza akasema " Dina 
ataniliha leo jioni!" ('Dina' ni jina la paka 
wa Elisi.) " Ewe Dina laiti ungekuwa nami 
kwa wakati huu ! Lakini hewani hakuna pa- 
nya ! Labda ungependa kukamata popo kama 
ungekuwa hapa ! Je, paka hula popo ? Si- 
jui." Macho yake Elisi yahkuwa mazito kwa 
usingizi, akaweweseka akawa kila mara ana- 
sema '' Paka hula popo " ? " Paka hula po 14 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

po " na mara kwa mara " Popo hula paka " ? 
'' Haidhuru nikisema paka hula popo au niki- 
sema popo hula paka, mamoja kwangu, maana 
mimi sijui kuyajibu maswali haya." 

EHsi akajiona amelala usingizi, akaota ya 
kwamba alikuwa akitembea pamoja na Dina, 
akamshika mkono akamwuliza sana akisema 
" Sasa Dina niambie kweli, unapenda kula 
popo ?" 

Kwa ghafula EHsi akajiona ameamka tena, 
naye amefika mwisho wa kisima; pana majani 
mengi sana makavu; na hapa kukawa mwisho 
wa kuanguka kwake. Elisi hakuumiwa hata 
kidogo, akaondoka mara moja akainua macho 
yake, lakini juu hakuona ila giza tu, na mbele 
yake pango liliendelea; na tahamaki akamwona 
yule sungura mweupe akitangulia kwa haraka. 
Elisi akajipa moyo, akapiga mbio sana apate 
kumkaribia, lakini alipokuwa karibu kabisa 
sungura akazunguka pembe ya njia, EKsi asi- 
mwone tena, bah alimsikia mbah kidogo aki- 
sema " Ole wa masikio yangu na mkia wangu ! 
nitakuwa nimechelewa sana " EUsi akazunguka 
pembe lakini sungura akawa ametoweka kabisa. 
Sasa yule mtoto akajiona yumo katika chu- 
mba kikubwa, chembamba, chenye dari fupi; 
kiliangazwa na taa zilizotundikwa darini, na 
katika kuta za chumba ilikuwamo milango 
mingi sana. Elisi akajaribu kufungua kila 
mlango, lakini yote ilikuwa imefungwa. PANGO LA SUNGURA 15 Kati kati ya chumba akaona meza ndogo ya 
kioo yenye miguu mitatu, na juu yake upo 
ufunguo wa dhahabu mdogo sana. EHsi aka- 
furahi akasema " Sasa naweza kufungua mi- 
lango," akajaribu sana asiweze, ufunguo mdo- 
go na tundu kubwa, akakata tamaa. Mwisho 
akaona mlango mdogo kabisa ambao hajapata 
kuuona, akainama akatia ufunguo katika tundu, 
na tazama ukafaa ! Elisi akafungua ule mla- 
ngo mdogo, akapiga magoti akachimgulia nda- 
ni. Kulikuwa na pango kama la panya, na 
mwisho wa pango kulikuwa bustani nzuri ka- 
bisa, akatamani sana kutoka chumbani mle 
alimokuwamo kwenye giza, ili afike kwenye 
jua na maua na chemchemi bustanini; lakini 
hakuweza hata kupitisha kichwa pangoni, aka* 16 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

sema " Kama ningeweza kiijipimguza kuwa 
nyembamba mfano wa bomba ya baisikeli 
ningeweza kuingia bustanini." (Wafahamu 
Msomaji, ya kuwa jinsi mambo mengi ya ajabu 
yalivyomtokea hata Elisi alidhani kwamba 
kwake yeye kila neno HUweza kutokea.) 

Elisi akarudi mezani, na sasa akaona chupa 
ndogo juu yake, na shingoni limefungwa kara- 
tasi kwa uzi, na juu ya karatasi imeandikwa 
" Uninywe." Elisi alikuwa mtoto mwenye 
akili, akasema, " Labda ni sumu " kwanza 
nitafute neno " ' sumu ' "; akatafuta sana lakini 
hakuliona, akafungua chupa akaionja kidogo 
dawa iliyokuwamo ndani yake; ladha yake 
tamu kama embe au nanasi au asali, akainywa 
upesi. 

Mara Ehsi alipokwisha kunywa dawa aka- 
jiona kuwa amepungua kimo, akafumba macho 
akaogopa kidogo, akasema " Labda nitatoweka 
kabisa kama nuru ya mshumaa inapozimwa." 
Ahpokwisha pungua aHfumbua macho, akajita- 
zama sana, urefu wake uhkuwa kama kuku; 
akasema " Nitaweza kuingia bustanini sasa 
hivi " Lakini, maskini EUsi, ahshindwa kabisa, 
kwa kuwa amesahau ule ufunguo mdogo wa 
dhahabu, aUuacha mezani; yeye sasa mdogo, 
hakuweza kufika mezani, aUjaribu sana ku- 
panda mguu wa meza baU aUshindwa kwa ute- 
lezi wake, na aUpochoka kwa kujitahidi aUkaa 
kitako akaUa sana; badaye akajilaumu aka- PANGO LA SUNGURA 17 senia " Basi, tulia sasa, haina faida katika kulia, 
nakuonya unyamaze upesi." Elisi ilikuwa de- 
sturi yake kujipa mashauri mazuri, ingawa 
mara nyingi hakuyafuata. Mtoto akazidi ku- 
jiambia " Faida gani kusema peke yangu " ? 
Mara EUsi akaona kisanduku chini ya meza, 
ndani yake uHkuwamo mkate mdogo, na ka- 
tika ule mkate yameandikwa maneno wazi 
wazi, kwa herufi zilizofanyizwa kwa chembe za 
mtama: " Unile." Ehsi akasema " Ni heri 
niule, halafu nitaona matokeo yake yataka- 
vyokuwa; labda utaniongeza urefu tena kama 
bomba ya baisikeh, nipate kutwaa ufunguo, na 
ukinipunguza zaidi nitaweza kutambaa chini 18 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

ya mlango kama mdudu, niingie bustanini." 
Akala kidogo ule mkate, akaweka mkono 
kichwani apate kuona wakati akipanda au aki- 
shuka, akashtuka kuona urefu wake ule ule, 
akacheka akasema " KweH mkate si dawa ya 
kugeuza mwOi, lakini hapa mahali pa ajabu, 
sina haja ya kushangaa nikigeuzwa na mkate." 
Akazidi kula hata akaumahza. 
SURA II 

KIDIMBWI CHA 
MACHOZI 

Elisi akapaza sauti 
akasema " H a p a 
mambo yote yana- 
zidi kunishangaza, 
kumbe najiongeza 
urefu kama bomba 
ya baisikeli kubwa 
kupita zote " ! Aka- 
inamisha m a c h o 
akajaribu kuvita- 
zama vidole vyake 
vya miguu, akavi- 
ona viko mbali sana, 
akasema " Kwa 
herini miguu, labda 
hatutaonana tena, 
nitawapeni zawadi 
wakati wa siku- 
kuu." Akacheka akasema 
kila neno " ! 

EUsi akajipiga kichwa darini, urefu wake 
ulikuwa kama wa watu wawili wakubwa, aka- 

19 Sasa nitapuuza 20 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

twaa ule ufunguo mdogo wa dhahabu, akaenda 
upesi kwenye mlango wa bustani. Maskini 
Elisi ! Baada ya kujitahidi sana aliweza kuu- 
karibia mlango, akalala kifudifudi akatazama 
kwa jicho moja bustanini, lakini kuingia haku- 
weza; akakata tamaa kabisa, akakaa kitako 
akalia sana, akajUaumu tena akasema " Ni aibu 
kabisa kulia namna hii, wewe mtoto mkubwa 
sasa, nawe walia kama mtoto mchanga, tulia 
mara moja " Walakini akazidi kulia akatoa 
machozi mengi sana, hata yakatosha kujaza 
mitungi ishirini, akawa amekaa katika kidi- 
mbwi cha maji. 

Badaye kidogo Elisi alisikia mashindo ya 
miguu midogo njiani, mbali kidogo, akajifuta 
machozi apate kumwona yu nani ajaye. Ku- 
mbe ni Sungura Mweupe aliyekuwa akirudi, 
amevaa nguo za umalidadi wa Kizungu, ame- 
shika mkononi mwake upepeo na kofia, anapiga 
mbio akinungunika na kusema " Atakasirika 
sana nikimkawilisha." Elisi, kwa sababu ya 
hali yake mbaya, na katika kukata tamaa 
kwake alikuwa tayari kumwomba msaada mtu 
ye yote, basi alipomkaribia Sungura alisema 
kwa hofu na kwa sauti ndogo " Shikamoo 
Bwana Sungura, Tafadhali ..." Sungura 
akashtuka sana hata akaangusha vitu alivyo- 
kuwa navyo, akakimbia upesi gizani. 

Mle chumbani alimokuwamo Elisi mlikuwa 
na joto kidogo, kwa hiyo alitwaa upepeo wa KIDIMBWI CHA MACHOZI 21 sungura, aliouangusha akaanza kujipepea, aka- 
jizungumza tena akisema " Ole wangu, hii ni 
siku ya ajabu ! Jana mambo yalikuwa sawa 
sawa, labda niligeuzwa usiku, nadhani ya ku- 
wa nimesahau yote niliyofundishwa chuoni." 
Akajaribu kusoma kwa moyo mashairi aliyo- 
jifunza zamani kidogo, akanena: 22 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

Kwa nguvu sana Mamba 
naling'arisha kila gamba 
Katika mto akang'aa 
Yu safi sana yule Mamba 

Na Mamba alichekelea, 
Akatandika kucha zake. 
Samaki walipotembea 
Wakahesabu meno yake. Key g. 
: j : S| I d : d I s : s I d : d I s : s I d : d I r.d : r.r 

Kwa ngu-vu sa-na Mam-ba a - na-ling'-a-ri-sha ki-Ia 

n : n I : s | l.s : f.n | r.n : f.s | n.f : n.r | d : s, 
gam-ba Ka - ti - ka m - to a - kang'-aa Yu 

l,.s, : l,.t, I d : r I d : d I : II : I : s, 
sa-fi sa-na yu - le Mam - ba. Na 

d : d I s .s : s .s I d : d | s : s | d : d | r .d : r .r 
Mam-ba a-li-che-ke - le - a, A- ka - tan - di - ka ku-cha 

n : n I : s | l.s : f.n | r.n : f.s | n.f : n.r | n : s, 
za-ke. Sa - ma - ki wa - li - po-tem-be-a Wa- 

l,.s, : l,.t, I d : r | d.r : n.f | s : s | l.s : f.n I r.n : f.s 
ka-he-sa-bu me-no ya - ke. . . Sa - ma - ki wa - li - 

n.f : n.r I d : s, | 1, .s, : 1, .t, | d : r | d : d | : | 
po-tem-be-a Wa - ka-he-sa-bu me-no ya-ke. KIDIMBWI CHA MACHOZI 23 

Kwa bahati njema wakati ule akaona ki- 
chwa na mkono, akashangaa kuona ya kuwa 
amevaa ile kofia ndogo ya Sungura, akasema 
" Nawezaje kuivaa kofia ndogo namna hii, 
ikiwa kimo changu ni kama kile cha watu wa- 
wiM ? Labda sasa nimepungua tena." Akao- 
ndoka akaenda mezani apate kujipima penye 
mguu wake; na kumbe, urefu wake ulikuwa 
kama wa mtungi, tena alikuwa anazidi kupu- 
ngua; akatafuta sababu ya kupungua kwake, 
akaona ya kuwa iUkuwa ule upepeo wa Sungura 
aUoushika, akauangusha upesi asizidi kupu- 
ngua, akasema " Bahati kubwa ! Kama ni- 
ngaUendelea kuushika ningalitoweka kabisa." 
EHsi akaogopa kidogo, lakini ahfurahi ya 
kuwa maisha yake hayajaisha bado, akasema 
" Vema, sasa nitakwenda bustanini." Akapiga 
mbio akafika mlangoni, lakini umefungwa ka- 
ma zamani, na ufunguo upo vile vile mezani. 24 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

Akalia sana akasema " Mambo yamezidi kuwa 
mabaya tena ni mara ya kwanza katika maisha 
yangu kuwa mdogo." Aliposema maneno ha- 
ya miguu yake ikateleza akaanguka akatumbu- 
kia katika maji ya chumvi mpaka kidevuni; 
kwanza alidhani ya kuwa ameanguka baharini, 
kisha akafahamu ya kwamba yale maji ya 
chumvi ndiyo kile kidimbwi cha machozi yali- 
yomtoka alipokuwa na urefu kama watu wawili, 
akasema " Adabu ya kulia ndio kufa ndani 
ya machozi !" 

Kwa ghafula Elisi akasikia kitu kinaruka 
majini, akaogelea karibu kidogo apate kuki- 
ona, kwanza alidhani ni kiboko, kisha akaku- 
mbuka udogo wake akaona ya kwamba ni 
panya tu, aliyeanguka majini kama yeye mwe- 
nyewe. 

Elisi akasema kimoyomoyo akinena " Labda 
inafaa kusema naye, ikiwa sungura wanaweza 
kusema katika nchi hii, bila shaka panya nao 
wanaweza; Hebu ! Nijaribu !" Akapaza sauti 
akasema " Ewe Panya, nchi kavu iko wapi ? 
Nimechoka kuogelea." Panya akamtazama 
mtoto kwa makini, akakonyeza jicho, bali ha- 
kujibu. EUsi akasema moyoni " Labda hasi- 
kii Kiswahili, nitasema Kiingereza." Hakujua 
ila maneno machache ya Kiingereza, akasema 
kwa sauti kuu " Where is my cat ?" (Maneno 
haya ndiyo ya kwanza katika kitabu chake 
cha kujifunza Kiingereza, tafsiri yake " Yuko KIDIMBWI CHA MACHOZI 25 

wapi paka wangu ?") Aliposikia maneno haya 
panya akaruka akatoka katika maji, akitete- 
meka kwa hofu; Elisi akasema " Niwie radhi 
Panya, nilisahau kabisa ya kuwa hupendi pa- 
ka." Panya akajibu kwa sauti nyembamba 
akasema " Kweli sipendi paka; je, wewe unge- 
wapenda paka kama ungekuwa kama mimi ?" 
Ehsi akajibu akasema " Ningekuwa kama we- 
we labda nisingewapenda, lakini nadhani unga- 
limpenda paka wangu, kwani ni mpole kabisa, 
jina lake Dina. Kazi yake ni kukaa kitako, 
kutoa ngurumo na kujiramba, napenda sana 
kumbembeleza naye ni fundi kabisa wa kuka- 
mata panya. . . . Niwie radhi ! Nimesahau." 
Panya alikuwa akitetemeka sana, EUsi aka- 
mwonea hurumu akasema '' Tusiendelee ku- 
zungumza juu ya paka." Panya akajibu aka- 
sema " Wasema Sisi tusiseme habari za paka; 
kwangu mimi simtaji hata jina lake, watu wa 
kabila langu huchukia kabisa paka, wanyama 
wabaya, hawana adabu, wakah, nisisikie 
tena hata jina hilo!" EHsi akajibu akasema 
"Vema, sitahtaja tena. Tuzungumze mambo 
menginje, je, wapenda mbwa ?" Panya haku- 
jibu, EUsi akaendelea kusema " Pana mbwa 
mzuri sana anayekaa penye nyumba yetu, 
nitapenda kukuonyesha, ana macho makubwa 
mazuri sana, rangi yake kama udongo, na 
kama ukitupa mpira anaudaka, bwana wa 
mbwa huyo anamsifu sana, asema ni mbwa 26 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU wa kufaa sana kuwafukuza panya wote nyu- 
mbani." 

Panya akaogelea upesi kumwacha Elisi, na 
kwa hiyo naye akatambua ya kuwa amemwu- 
dhi, akamwita akasema " Ee Panya mpenzi 
rudi ! Natoa ahadi ya kuwa siwezi kusimulia 
tena habari za paka wala mbwa." 
Aliposikia haya panya akarudi pole pole, 
akasema kwa sauti ndogo " Twende nchi kavu 
kisha nitakuhadithia habari za maisha yangu, 
upate kufahamu jinsi ninavyowachukia paka 
na mbwa." 

Bila shaka wakati wa kutoka kidimbwini 
uMkuwa umefika, maana wanyama wengi wa- KIDIMBWI CHA MACHOZI 27 

mekusanyika majini, waliotumbukia humo ka- 
ma Elisi na Panya. 

Palikuwa na bata mmoja, Doda mmoja, 
lauri mmoja, Tai mmoja na wanyama wengine 
wa ajabu. 

Elisi akatangulia, wakaogelea wote mpaka 
nchi kavu. SURA III 

SHINDANO LA KAKA 

LiLiKUWA kiindi la ajabu sana lililokuwapo 
pwani; ndege wote manyoya yao yalikuwa 
yamelowa, na maji yalikuwa yanatiririka ka- 
tika ngozi za wanyama; wote wamenuna kwa 
hali yao mbaya; wote wakahitaji kukauka, 
kila mmoja akapiga kelele kupita wenzake ka- 
tika kutoa mashauri ya njia za kuweza kukau- 
ka. Ehsi akafanya kelele kupita wote, ha- 
swa aUshindana kwa maneno na yule Lauri, 
mpaka mnyama huyu akakasirika kabisa aka- 
kataa kusema, ila maneno yale, aliyoyasema 
mara nyingi sana, ndiyo: '' Mimi nimekaa du- 
niani miaka mingi kupita wewe, kwa hiyo mimi 
najua zaidi." EHsi akamwuliza umri wake, 
lakini akakataa kabisa kumwambia. 

Panya alichoka akamwuHza EHsi akasema 
" Waendeleaje mwanangu ? Umekwisha kau- 
ka?" EHsi akajibu "Sijakauka hata kidogo." 
Doda akapaza sauti akasema " Kwa hiyo nawaa- 
muru wote wafikiri shauri jingine la kufaa, kwa- 
ngu mimi shauri ni kupiga ' Shindano la Kaka.' " 
EHsi akauHza akasema " Shindano la Kaka ni 
nitii?" Doda akasema "Namna ilyo bora ya 
kueleza kitu ni kukitenda." 

28 SHINDANO LA KAKA 29 

Kwanza Doda akapiga mstari chini kwa dua- 
ra mkubwa, hii ndiyo njia ya kutembelea, 
kisha wote wakasimama mstarini, huko na 
huko, wakakimbia wanapopenda, kwa hiyo 
ihkuwa si rahisi kujua kikomo cha shindano 
hilo; walakini wote walipiga mbio kwa nusu 
saa, na walipokuwa wamekwisha kukauka Do- 
da akasema kwa sauti kuu " Shindano lime- 
kwisha." Wote wakatuha wakamsogelea Doda 
wakitweta, wakamwuhza wakisema " Tuambie 
Doda, nani aliyeshinda ?" Doda akakaa aka- 
fikiri saaaaaana, kidole kinywani, na wote wa- 
likuwa wamengoja, mwisho Doda akapiga ke- 
lele kwa furaha akasema " Wote wameshinda, 
wote watapata tuzo." Kwa sauti moja wa- 
nyama wakauliza wakasema *' Nani atakaye- 
toa tuzo " ? Doda akajibu " Huyu." Akamwe- 
lekezea kidole EUsi, makutano ukamgeukia 
Elisi wakasema " Tuzo ! Tuzo ! Twataka 
tuzo." Elisi akaogopa kidogo lakini ahku- 
mbuka ya kuwa zamani kidogo aUfunga senti 
chache za moja moja katika pembe ya shiti 
yake, akaifungua fundo upesi, akaona ya 
kwamba kwa bahati aUkuwa na senti za kuto- 
sha kumpa kila mtu moja; akazitoa kwa uta- 
ratibu, wote wakapendezwa sana. Panya aka- 
mwambia EMsi " Wewe pia, lazima upate tuzo." 
Doda akaitikia " Ndio, lazima upate tuzo vile 
vile; je, unazo nyingine fundoni mwa kanga " ? 
EUsi akajibu " Sina, ila pete tu " ! Doda aka- 30 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU nena * ' Itaf aa, nipe. ' ' Elisi akampa ndege ile pete, 
huyu akamrudishia kwa heshima kuu akasema 
" Pete hii iwe na kibah kwa Mama." Na ahpo- 
kwisha kusema maneno haya wote wakapiga 
makelele ya kushangiUa. EHsi akafikiri kuwa 
matendo haya hayana maana, lakini akawasa- 
limu wanyama akapokea pete, akaivaa kidolini. 
Elisi akamwita Panya akamwambia kwa 
sauti ndogo akasema " Ewe Panya zamani ki- SHINDANO LA KAKA 31 dogo uliahidi kunisimulia hadithi ya maisha 
yako, na kwa nini wachukia sana wanyama 
wa namna fulani (Siyataja majina yao)," Panya 
akamjibu Ehsi kwa huzuni akasema " Hadithi 
yangu ndefu sana. Katika nchi yetu desturi 
ni hii: Fulani akiwa na mkia mrefu, husemwa 
ana bahati ya kuishi siku nyingi, tena ana ruksa 
kusimuHa hadithi ya maneno mengi; mkia wa 
fulani ukiwa mfupi, maisha yake mafupi pia, 
na hadithi yake lazima iwe na maneno macha- 
che tu. Katika nchi yangu ' Mkia ' na ' Ha- 
DiTHi ' ni neno moja, nikisema * Mkia wangu 
mrefu ' au ' Hadithi yangu ndefu ' maana ya- 
ke sawa sawa; na mkia wangu ni mrefu 
mno. 'Hadithi' au 'Mkia' wangu ni hii": — 32 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

"Mama yangu 
iia Paka na 
M bw a wa li - - 
kuwa rafiki. 
Mbwa akamshtaki 
mama yangu. A- 
kasema, wewe 
umeiba cba- 
k u 1 a c h a 
B w a n a w a - 
ngu wewe mwivi 
nitakushtaki kweli 
serikalini - - 
M wam uzi ak a - 
s ema *'K w eli 
Panya wewe mtu 
mbaya sana, wa- 
stahili kuuawa 
Mbwa na paka 
wamepewa ruk- 
sa kukurarua, 
Mbwa na Paka 
wakafurahi 
wakamkamat 
a mama 
yangu, wa- 
kamwua u- 
pesi, tena 
wakawa- 
kamata 
ndugu z*- 
ngu wote, 

mimi uilikaa peke 

yangu, nikihuzunika saaaana." SHINDANO LA KAKA 33 

Panya akajikatiza maneno akamwambia Elisi 
akasema " Husikilizi ! Unafikiri T iini ?" Elisi 
akajibu kwa unyenyekevu akasema " Sifikiri 
kitu Panya, nasikitika sana, tafadhali uni- 
samehe." Lakini yule mnyama alikasirika ka- 
bisa akaondoka, Elisi na wanyama wengine 
wote pia wakamwita, lakini alikataa kurudi, 
akazidi kukaza mwendo. 

Elisi alisema " Dina angekuwapo hapa ange- 
mrudisha upesi Panya." Lauri akauUza " Dina 
nani"? EHsi akajibu kwa furaha akesema 
" Dina ni paka wangu, ni hodari kabisa kuka- 
mata panya, tena anaweza kukamata ndege, 
ni paka mwenye akili nyingi." 

Maneno yake Elisi yahwatia hofu wale we- 
nzake ndege; wengi wakaondoka wakaenda 
mara moja bila kuaga, wengine wakasema 
" Baridi kali sana, lazima turudi nyumbani." 
Hawakumtaka EHsi awasindikize. Kwa saba- 
bu mbaU mbaU wote wakaenda zao; Efisi 
akabaki peke yake kabisa, akasema kwa huzuni 
" Sasa nasikitika ya kuwa nihsema habari za 
Dina, imebainikia ya kwamba wenyeji wa nchi 
hii wanamchukia, ingawa ni paka mwema kupita 
wote. Ee Dina nina haja nawe sasa, je, sitakuona 
tena ?" EHsi akatoa machozi, maana amekuwa 
mpweke, mwenye huzuni, walakini baadaye 
kidogo aHsikia tena mashindo ya miguu midogo 
njiani, akatuHa akidhani kuwa iHkuwa Panya 
aHyekuwa anarudi. Kumbe haHkuwa yeye ! 

3 AIW C SURA IV 

NYUMBA YA SUNGURA 

Alikuwa Sungura Mweupe aliyekuwa akirudi, 
akitafuta huko na huko ahmokuwa akienda, 
kana kwamba amepotelewa na kitu, akanu- 
ng'unika akisema " Mama Mkubwa ! Mama 
Mkubwa ! Maskini miguu yangu, masikio na 
midomo yangu ! Bila shaka nitakatwa kichwa ! 
Nimeviangusha wapi ?" Mara EHsi akabahati- 
sha ya kuwa ahkuwa anatafuta upepeo na 
kofia yake, ahyoangusha zamani kidogo; aka- 
msaidia katika kutafuta kwake, baU hakuviona. 
Mahali pamebadihka tangu kuogelea kwake 
EHsi kidimbwini, na kile chumba kirefu chenye 
meza ya kioo, na mlango mdogo kimetoweka 
kabisa. 

Kitambo kidogo Sungura akamwona EHsi, 
ambaye aHkuwa akitafutatafuta, akamwita 
kwa hasira akisema " Ewe Meriana, wafanyaje 
hapa ? Rudi nyumbani upesi, kaniletee upe- 
peo na kofia nyingine." 

EHsi akaogopa sana akakimbia kwa hima 
njia aHyoielekeza Sungura, hakukaa wala ha- 
kumwonyesha Sungura kosa lake, na aHpo- 
kuwa akitembea aHsema moyoni " Amenidhani 
mimi ni yaya, atashtuka atakapoona kuwa si- 

34 NYUMBA YA SUNGURA 35 

ye, lakini afadhali nimletee upepeo na kofia." 
Kabla hajamaliza maneno akaona nyumba 
ndogo safi, na mlangoni imeandikwa na herufi 
za shaba: " Bwana S. Mweupe." 

Elisi hakupiga hodi, akaingia nyumbani aka- 
panda ngazi kwa hofu, akadhani ya kuwa ata- 
kutana na huyu yaya mwenyewe, atupwe nje 
kabla hajapata upepeo na kofia ya Sungura. 
Elisi alicheka alipofikiri ya kwamba ametumwa 
na sungura, akasema " Nitakaporudi kwetu 
labda Dina atanituma pia." Akaingia ndani 
ya chumba kidogo, safi kabisa, chenye dirisha 
na meza; na mezani akaona upepeo na kofia 
ndogo. 

Ehsi akafurahi, basi alipokuwa katika kuvi- 
twaa, aliona chupa mezani, na ingawa haina 
cheti cha maelezo kama cha ile ya kwanza, au 
neno " uninywe " aliinywa dawa iliyomo ndani, 
akasema " Sasa nitapata mambo gani ?" Maa- 
na Elisi alifahamu siku zile kuwa anywapo 
cho chote hufikiwa na mambo mbali mbali. 
Ehsi akasema " Labda dawa hii itaniongeza 
urefu, nimechoka kuwa mbilikimo namna hii !" 
Dawa ilimfaa upesi kabisa, na kabla hajaweza 
kutoka chumbani alijidunda kichwa darini, 
akairudisha chupa mezani akasikitika ya kuwa 
amekunywa nyingi, sababu alikuwa hajaacha 
kukua, akakaa chini akanyosha mkono diri- 
shani, na mguu katika bomba la moshi, apate 
kuwa na nafasi, akasema " Nitokeje sasa ?" 36 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU Kwa bahati wakati ule iile nguvu ya dawa 
ilipungua, lakini alikuwa hana wasaa hata wa 
kugeuka, amebanwa kabisa, hakujua njia ya 
kuokoka, akasema moyoni " Kwetu maisha 
yangu mazuri kupita ya hapa, huko siku- 
punguka wala sikuongezeka kila nilapo au 
niywapo, tena situmwi na sungura wala pa- 
nya. Sasa nasikitika ya kuwa nimemfuata 
sungura pangoni, nasikitika kama sisikitiki. 
Zamani nilisoma hadithi za namna hii, siku- 
dhani ya kuwa mimi nitakuwa mtu wa hadithi. 
Ni heri kiandikwe kitabu juu ya habari hizi, 
au labda nitakiandika mwenyewe nitakapo- 
kuwa mtu mzima." Kabla hajamaliza kusema 
akasikia sauti ya Sungura nje, aliyekuwa aki- NYUMBA YA SUNGUEA 37 mwita yaya, akisema " Ewe Meriana, niletee 
kofia upesi !" Elisi akasikia mashindo ya mi- 
guu midogo ngazini, akatetemeka kwa hofu. 'fl ^jNWewPE 
akasahau ya kwamba yeye ni mkubwa kabisa 
kuliko Sungura na wenzake, wala hakuna 
haja ya kuogopa. Sungura Mweupe akafika 
mlangoni akajaribu kuufungua, bali alishi- 38 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

ndwa, maana Elisi alikuwa ameuzuia kwa 
kisigino, mnyama akasema " Vema, nitaingia 
dirishani." Elisi akajibu moyoni akasema 
" Haingii, nitamzuia." Akangoja mpaka aka- 
msikia nje, chini ya dirisha, akatoa mkono 
kwa kumdaka, lakini alimkosa, akasikia ki- 
shindo kama cha kuanguka kitu penye mitungi 
mingi, kikaivunjavunja, tena alisikia yowe 
ndogo, na halafu sauti kali, (Ilikuwa ile ya 
Sungura Mweupe.) akiita akisema " Ewe Patriki, 
umekwendapi ?" Kisha Elisi akasikia sauti 
asiyopata kusikia, ya mtu mmoja akijibu aki- 
sema " Nipo Bwana, nafukua matunda." Su- 
ngura akasema " Maana yake nini kufukua 
matunda ? Mjinga we ! Njoo upesi unisaidie 
nitoke katika mitungi." Elisi akasikia tena 
kelele za vyombo vikivunjika; Sungura aka- 
sema " Sasa, niambie Patriki, waona nini 
dirishani ?" 

" Naona mkono Bwana." 

" Haiwezekani ! Sijapata kuona mkono mku- 
bwa namna hii. Mpumbavu we ! Tazama 
umeenea dirisha lote !" 

" Kweli Bwana, lakini ni mkono ujapokuwa 
mkubwa." 

" Vema, Lakini unafanya nini dirishani ? 
Hauna ruksa kuwapo huko, nenda kauondoe, 
kautupe." 

" Mimi naogopa Bwana, tena sitaki kuutupa." 

" Fuata maneno yangu upesi, mwoga we !" NYUMBA YA SUNGURA 39 Elisi akataka tena kumkamata Sungura lakini 

akasliindwa, alisikia mayowe mawili memba- 

mba, na tena ke- 

lele za mitungi 

inay ovunjika, 

akasema kimoyo- 

moyo " Mitungi 

mingi iko kule, 

haiwezekani mimi 

kuvutwa katika 

dirisha, lakini ni- 

mechoka kulala 

hapa." Akasiki- 

liza sana, haku- 

sikia k i t u , i 1 a 

kimya t u, a k a- 

ngoja kwa dakika 

chache, h a 1 a f u 

akasikia s a u t i 

nyingi za watu wa- 

liokaribia ; mara 

kwa mara maneno 

yao yahfuatana, 

ndiyo: "Ikowapi 

ngazi ?" " Lete 

mbih, kazifunge 

pamoja." " We- 

we, shika kamba hii." 

"Mathubuti kabisa." 

bombani ?" " Si mimi." 
" Itafaa, ina imara." 
Nani atakayetelemka Mimi sitaki. 40 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

*' Mimi naogopa." " Mimi nakataa." " Wi- 
lyam, hii ni kazi yako, umetumwa na Bwana, 
panda upesi I" Wakumbuka Msomaji ya kwa- 
mba mguu wa Elisi ulikuwa bombani, kwa 
hiyo aliposikia shindo darini alisema moyoni 
" Wilyam ndiye atakayeshuka bombani, hja- 
pokuwa jembamba nadhani ya kuwa naweza 
kumpiga teke." Akaukweza mguu kama ali- 
vyoweza, akangoja mpaka akasikia mnyama 
bombani, ndipo akapiga teke kwa nguvu. 
Hakujua hata kidogo ni mnyama wa kabila 
gani. 

PaHkuwa na ghasia kabisa nje, EUsi aka- 
sikia maneno haya: " Tazama Wilyam !" " Loo 
anaruka kama ndege !" " Uchawi gani huu ?" 
" Mkamate Patriki we." " Mimi nitampa da- 
wa." "Mshike kichwa." " Waonaje Kaka." 
" Mambo gani umepata ?" " Tuambie yote." 
Wilyam akajibu kwa sauti ndogo akasema 
" Mimi siwezi kueleza, kiti kikubwa, kama 
mguu wa binadamu kimenipiga nilipokuwa 
bombani, nikatoka kama mshale uUotoka ka- 
tika upindi." Wenzake wakamjibu " KweU, 
umeruka kama mshale." 

Sauti ya Sungura Mweupe ikasikilizana, wote 
wakanyamaza; Bwana Sungura akasema " La- 
zima tuichome nyumba hu." EUsia kapaza 
sauti sana akasema " Mkichoma nyumba nita- 
mtuma Dina awakamate ninyi nyote." Mara 
wote nje wakatuUa, baadaye wakaanza tena NYUMBA YA SUNGURA 41 

kutembeatembea. Simgura Mweupe akasema 
" Kikapo kimoja kitatosha kwanza." Elisi aka- 
fikiri "Ndani ya kikapo mna nini?" Mara 
akatambua, maana mawe mengi madogo yali- 
ingia dirishani, machache yakampiga usoni; 
akasema " Tulieni sasa hivi." Mara watu wa nje 
wakasita kuyatupa. Elisi akayatazama mawe 
yaliyokuwa chini, akaona ya kuwa yame- 
geuka kuwa pelemende, akadhani akasema 
moyoni " Nikila pelemende labda urefu wangu 
utapungua." Akaila moja, akafurahi sana kwa 
kuwa amepunguka mara, akawa mdogo wa 
kuweza kuondoka; akatoka nyumbani. 

Nje palikuwa na makutano ya wanyama na 
ndege; Wilyam alikuwa Mjusi, alikuwa kati 
kati ya kundi, akibembelezwa na Komba 
wawili, waliokuwa wakimpa dawa. 

Walipomwona Elisi wanyama wote wakapiga 
kelele sana, wakafukuza upesi wapate kumka- 
mata; Elisi akapiga mbio akawashinda, aka- 
jificha kati ya miti mikubwa mizuri sana 
mwituni. 

Elisi alitembeatembea mwituni, akasema 
" Kwanza afadhah nifikiri jinsi ya kutengeneza 
urefu wangu, niwe sawa sawa, kisha niingie 
katika bustani niliyoiona zamani kidogo." Ma- 
shauri haya yahkuwa mazuri lakini EHsi haku- 
jua jinsi ya kuyatimiza. 

Ghafula yule mtoto alishtuka kusikia kilio 
cha mbwa juu yake, akainuisha macho akaona 42 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 'mtoto wa mbwa aliyekuwa akimtazama kwa 
makini; mbwa akanyosha mguu mmoja aka- 
jaribu kumgusa mtoto; Elisi akapiga uruzi 
akasema " Basi mbwa, pole pole !" Lakini 
aliogopa sana akasema " Akiwa na njaa ata- 
nila." Akatwaa fimbo akacheza na mbwa NYUMBA YA SUNGURA 43 

akijilinda nyuma ya maua yenye miiba, aka- 
sema kimoyomoyo " Ni kama kucheza na 
tembo !" Akawa na hofu kuwa atavunjika 
na miguu yake, lakini hakuthubutu kukimbia 
mpaka mbwa akawa amechoka kabisa, ahpo- 
kwisha kuchoka mbwa akalala akitweta sana, 
akafumba macho; mara Elisi akakimbia, na 
hakukaa mpaka kilio cha mbwa kilisikilizana 
kwa mbali sana. 

Ehsi aUpumzika penye kivuli cha njugu, 
akajipepea kwa jani moja, akasema " Wala- 
kini ni mbwa mzuri sana, bah mimi mdogo, 
sikuweza kumtiisha, lazima nijiongeze urefu, 
lakini hapa chakula hakuna, sijui nitakacho- 
kula." Elisi akatafutatafuta bila kuona cha- 
kula hata kidogo. 

Mara Ehsi ahona uyoga, urefu wake kama 
yeye mwenyewe, akatazama chini yake, hala- 
fu akataka kutazama juu ya ule uyoga, aka- 
chuchumia akaona juu Mdudu mkubwa wa 
rangi ya buluu, ahkuwa amekaa amejikumbatia 
akivuta kiko cha Kihindi; hakujishughuHsha 
na EUsi kwa neno lo lote. 
SURA V 

MASHAURI YA MDUDU 

Elisi na yule Mdudu walitazamana kwa dakika 
chache, bila kusemezana. Mwisho Mdudu aU- 
toa kiko kinywani akasema kwa ulegevu " Ja- 
mbo mwanangu, nani wewe ?" EHsi akajibu 
kwa hofu kidogo akasema " Sijui Bwana, 
asubuhi, nilipoondoka nihjijua, lakini tangu 
saa ile nimegeuka mara nyingi sana, na sasa 
labda ni mtu mwingine !" Mdudu akajibu 

44 MASHAURI YA MDUDU 45 

*' Sielewi, eleza tena." Elisi akasema " Siwezi 
kueleza, maana sijifahamu mwenyewe, lakini 
najua hili, ya kuwa ni vigumu sana kuwa na 
urefu mbali mbali katika siku moja." Mdudu 
akavuta kidogo akasema " Si vigumu." Elisi 
akajibu " Wewe mwenyewe kama utakuwa 
kama kipepeo utafahamu kuwa ni vigumu." 
Mdudu hakukubali akasema " La ! Hasha !" 
EHsi akajibu akasema " Labda sisi mambo 
yanatudhihirikia, lakini kwangu mimi naona ni 
vigumu kugeuka." Mdudu akamtazama Elisi 
kwa dharau akasema " Nani wewe ?" EUsi 
akakasirika akasema " Umeturudisha mwanzo 
wa mazungumzo yetu, nadhani ni juu yako 
kwanza kuniambie habari zako." Mdudu aka- 
mtazama akasema " Kwa nini ?" Elisi aka- 
shindwa kabisa kujibu, akaenda kidogo, lakini 
yule mdudu akamwita akasema " Rudi. Nina 
neno." Ehsi akakubaU akarudi. Mdudu aka- 
sema " Usikasirike. Basi." Elisi akazidi ku- 
kasirika akasema " Neno lako ndilo hili tu ?" 
Mdudu Mdudu akajibu " La." Yule mtoto 
akafikiri ya kuwa anayo nafasi, kwa hiyo 
akangoja, apate kusikia maneno ya Mdudu; 
akakaa kwa uvumilivu; muda wote huyu 
Mdudu alikuwa akivuta kiko kwa pole pole, 
halafu alinyosha mkono akaondoa kiko mdo- 
moni akasema " Je, wadhani kuwa umegeuka ?" 
Elisi akajibu kwa huzuni akasema " Kweli 
nimegeuka, kwa hiyo nasikitika sana, tena kwa 46 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU sababu hii siwezi kukumbuka elimu niliyoji- 
funza chuoni, na urefu wangu umwbadiHka 
mara nyingi." Mdudu akamtiisha Elisi kama 
mwalimu, akasema " Soma kwa moyo ' We 
mzee Baba Wilyam.' " Elisi akasimama wima 
akajifunga mikono nyuma, akanena 
" We mzee Baba Wilyam," 'kasema mwanake, 
" Nyeupe kabisa nywele, 
Kusimama kwa kichwa imekufalia ? 
Je, utacheza milele ?" 

Baba Wilyam 'kajibu " Katika utoto 
Nilihofu kudhuru ubongo, 
Bali sasa najua kichwani ni tupu, 
Nikazidi pindua mgongo." MASHAURI YA MDUDU 47 Key G. 

{] : n .pi I r : n .r | d : s, .s, | 1| : d . t, | 
" We m - zee Ba-ba Wil-yam," 'ka - se - ma mwan- 

{| d.d : d.r I n : n.n | fe : s.fe | n : n | 
a-ke, " N-ye - u - pe ka - bi - sa ny - we - le. {| u 

: n.n | f : n.r | d : tj .r | n, : r .t, | 
Ku-si - ma-makwa ki-chwai - me-ku-fa- II 1, : 1, I s, : d.n | r : d .r | d : d 
- li - a? Je, u-ta - che - za mi - le - le?' 
Mwana 'kasema " We mzee baba yangu, 
Kama nilivyosema zamani, 
Walakini ingia kwa kichwani chini 
Ni desturi ukija nyumbani." 48 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

Mzee akasema " Katika utoto 
Nilijilainisha mwili 
Kwa dawa katika sanduku za ehuma 
Na nitakuuza mbili." 
Kijana 'kasema " Wewe kibogoyo, 
Huwezi kula ila wali, 
Lakini wameza mbuzi mzima 
Jinsi gani ? Nijibu maswali." 

" Nilikuwa Mwamusi zamani kidogo, 
Na Mwamusi ni mtu wa cheo, 
Kila siku mashauri, na tayani mwangu 
Nguvu hukaa hata leo." MASHAURI YA MDUDU 49 

Kijana 'kasema " We mzee Baba Wilyam, 
Lakini najua, waweza 
Simamisha samaki mkubwa puani 
Namna gani mzee ? Nieleza." 

Mzee akasema kwa nguvu na ehuki 
" Nimejibu maswah matatu, 
Itatosha mwanangu uache ujinga, 
Nenda ! Nisikupige kiatu." 
Mdudu akasema " Maneno haya si sawa sa- 
wa." Elisi akajibu akasema " Hata mimi nao- 
na si sawa sawa kabisa." Mdudu akaitikia 
" Si sawa sawa hata kidogo." Wote wawili 
wakanyamaza muda wa dakika chache, hala- 50 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

fu Mdudu akasema " Wataka kuwa na urefu 
gani ?" Elisi akajibu " Habari za urefu ni 
mamoja kwangu, lakini sipendi kugeukageu- 
ka hivi. Umefahamu ?" Mdudu akajibu " Si- 
jui." EHsi akanyamaza kwa kuwa maisha 
yake yote hajapata kupingwa na maneno na- 
nma hii, akakasirika; Mdudu akamwuHza " Je, 
u radhi sasa ?" Elisi akajibu " Ningependa 
kuwa mkubwa zaidi kidogo, maana kuwa na 
urefu kama uyoga tu si vizuri." Mdudu aka- 
simama wima akasema kwa nguvu " Urefu wa 
uyoga ni kimo kizuri kabisa " (huu ndio urefu 
wa Mdudu mwenyewe). Elisi akapiga mguu 
akasema kwa hukumu " Mimi sijazoea kuwa 
mdogo." Akawaza ya kuwa vyumbe vya nchi 
ahyokuwamo hawakawii kuchukiwa. Mdudu 
akasema " Baadaye utazoea." Akatia kiko 
midomoni akavuta. EHsi akangoja kwa uvu- 
mihvu hata Mdudu ahposema tena. Mdudu 
akaendelea kuvuta tumbako, halafu akapiga 
mwayo mara mbih tatu, akajitetemesha, aka- 
shuka juu ya uyoga, akatambaa katika ma- 
jani; ahpokuwa akienda akasema " Upande 
mmoja utakuongeza, upande wa piH utaku- 
punguza urefu." EHsi akasema " Asante Mdu- 
du." Akanena kimoyomoyo " Pande za ni- 
ni ?" Mdudu akajibu kana kwamba anawaza 
tu, akasema " Pande za uyoga." Akatoweka 
mwituni. 

EHsi akakaa akautazama ule uyoga, apate MASHAURI YA MDUDU 51 

kutofautisha pande zake, kazi hii ilikuwa ngu- 
mu maana uyoga ulikuwa mviringo kamiH; 
akanyosha kabisa mikono akashika ukingo wa 
uyoga kwa mikono miwih akaumega vipande 
viwiH, kimoja katika mkono wake wa kulia na 
kingine katika mkono wa kushoto, akajiu- 
liza " Kipande kipi kitaniongeza, na kipande 
kipi kitanipunguza ?" Akala kidogo kile ki- 
pande cha mkono wa kuha, Kabla hajamaUza 
kula aUjipiga vidole vya miguu kwa kidevu; 
akaogopa sana, akaanza upesi kula kile kipande 
cha mkono wa kushoto kazi hii ilikuwa ngumu 
sana maana kidevu kilikuwa kimekaribia sana 
vidole vyake vya miguu, iHkuwa hakuna nafasi 
ya kutafuna, lakini kwa shida akaweza, aka- 
sema kwa furaha " Sasa kichwa kimeokoka." 
Lakini kabla hajamaHza kusema aHogopa tena 
kwa kuwa hakuweza kuona mabega, hata 
kidogo, aHpoinamisha macho hakuona kitu 
ila shingo tu; shingo iHkuwa refu sana kupita 
ile ya twiga, na shingo yenyewe iHtokeza juu 
ya majani ya miti, juu kabisa, kama mnazi 
katika mashamba. EHsi akafikiri " Majani yale 
ya nini ? Tena mabega yangu ya wapi ? Si- 
wezi kujiona, hata mkono." Alipokuwa aki- 
sema maneno haya aHnyosha mkono lakini ha- 
kuuona, aHona tikisiko la majani tu. Kwa 
sababu hakuweza kuufikisha mkono kichwani 
aHjaribu kuinamisha kichwa kifikie mikono, 
akaona furaha ya kuwa aHweza kuipindapinda 52 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

shingo kama mwili wa nyoka, akaona ule 
uwanda wa majani, na kumbe ulikuwa vilele 
vya miti tu. 

Ghafula ndege kubwa aliruka usoni mwake 
Ehsi, akampiga sana kwa mabawa, akasema 
kwa sauti nyembamba " Nyoka ! Nyoka !" 
Elisi akajibu kwa hasira " Usinipige hivi, mimi 
si nyoka." Lakini Ndege akazidi kufanya ma- 
tata na kusema " Nyoka ! Nyoka !" Akatoa 
machozi akasema " Kila mahali nimetafuta, 
lakini hapana mahali pa kuwafalia watoto wa- 
ngu." EHsi akajibu akasema " Sielewi hata 
kidogo." Ndege akasema " Nimejaribu ma- 
shina ya miti; nimejaribu dari za nyumba, ni- 
mejaribu maboma ya shamba, bah wale nyoka 
wabaya wamenifuata kila mahali." EHsi aka- 
zidi kushindwa, lakina hakumkatiza maneno 
ndege, mpaka alipokwisha kusema. Ndege 
akaendelea kunena akasema " Ni kazi kubwa 
kuangua mayai, tena imenilazimu kuyaHnda 
kutwa kucha, sikuupata usingizi tangu juma 
tatu, nimechoka kabisa." Elisi akaanza ku- 
fahamu akamjibu akasema " Nasikitika sana 
ya kuwa umesumbuka hivi." Ndege akasema 
" Wakati nilipouchagua mti mrefu kupita yote 
mwituni na nilipodhani ya kuwa mayai yangu 
yatakuwa salama mara nihmwona nyoka ah- 
yetoka mbinguni. . . . Ewe Nyoka ! Nenda 
zako." EHSi akajibu akamwambia " Mimi si 
nyoka, mimi . . . mimi . . . mimi. ..." Ndege MASHAURI YA MDUDU 53 

akasema " Sasa nani we ? Naona ya kuwa 
wajaribu kusingizia kitu." Elisi akajibu " Si- 
singizii; mimi binadamu." Ndege akamtazama 
Elisi akacheka akasema " Nimeona watoto 
wengi sana, lakini sijapata kuona mtu mwenye 
shingo refu kama yako, huwezi kukana ya 
kwamba wewe u nyoka, je, huli mayai ?" 
Elisi akajibu " Nala mayai, lakini ni desturi 
ya wanadamu kula mayai, kama ilivyo desturi 
ya nyoka." Ndege akasema " Sikusadiki, la- 
kini ikiwa kweli kwamba wanadamu wanakula 
mayai kama nyoka, basi mimi nawachukia 
kama nilivyowachukia nyoka." EHsi akajibu 
akasema " Mimi sitafuti mayai yako, hata kama 
ningetafuta nisingependa yako, wala mimi sili 
mayai mabichi." Ndege akatuHa akasema 
" Vema, nenda zako." Akarudi kiotani. EU- 
si akaendelea kuinamisha kichwa kama ahvyo- 
weza, ilikuwa kazi ngumu, maana mara kwa 
mara shingo yake ilikwama matawini. Mwisho 
akafaulu akakumbuka ya kwamba alikuwa 
ameshika vile vipande viwili vya uyoga. Akaa- 
nza kula, kimoja kwanza, kisha kingine mpaka 
urefu wake ukawa sawasawa, akajichangamsha 
akasema " Sasa limetimia shauri langu nusu 
yake, hlilobaki kwangu ni kuona bustani." 
Akatembeatembea mwituni. Kitambo kidogo 
EHsi akaona nyumba ndogo, kimo chake kihku- 
wa kama cha meza; akajiuliza " Nyumba ya 
nani hii ? Lakini haifai kabisa kupiga hodi. 54 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

maana mimi mkubwa ! Mwenye nyumba atao- 
gopa sana kama akiona jitu kama mimi ?" 
Akala kidogo kipande kile cha uyoga cha 
mkono wa kuUa, wala hakuthubutu kukaribia 
nyumba mpaka alipokuwa amejipunguza akawa 
na urefu wa inchi tisa. 
SURA VI 

NGURUWE NA PIUPILI 

Elisi alisimama akatazama nyumba muda 
wa dakika chache, akaona kuwa ilikuwa nyu- 
mba ya Kizungu, safi kabisa; na alipokuwa 
akisimama akaona askari aliyetoka mbio mwi- 
tuni; alimjua kuwa ni askari kwa ajili ya ma- 
vazi yake; lakini usu wake ulifanana na ule 
wa samaki. Askari Samaki akaenda mlangoni 
akabisha sana, akapiga hodi mara nyingi; 

55 56 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

mlango ukafunguliwa na askari mwingine mwe- 
nye uso wa chura, alitoka nyumbani. Elisi 
akasogea kidogo apate kusikia maneno yao. 
Askari wa kwanza alikuwa na barua kubwa 
sana, akampa askari wa pili kwa heshima 
akasema " Barua hii inatoka kwa Malkia Mzu- 
nguwapili, inakAvenda kwa Mama Mkubwa, 
ataka acheze Kriketi naye." Askari mwenye 
uso wa chura akayakariri maneno yale aka- 
sema " Barua hii inakwenda kwa Mama Mku- 
bwa, inatoka kwa Malkia MzunguwapiH, ataka 
acheze Kriketi naye." Askari wakasujudiana 
sana, na kwa hiyo EHsi ahcheka mno, akaki- 
mbia tena mwituni wasiweze kumsikia. AH- 
potazama tena ahona ya kwamba Askari Sa- 
maki aUkuwa amekwisha kwenda, na mwingine 
ahkaa penye mlango akitazama mbinguni ka- 
na kwamba ni mpumbavu; Elisi akaenda mla- 
ngoni akabisha akapiga hodi; Askari Chura ha- 
kumzuia, akamwambia " Unapiga hodi bure 
kwa sababu mbili; ya kwanza kwa kuwa sisi 
sote wawili tupo upande wa nje wa mlango; 
ya pili kwa kuwa wale waliomo ndani wana- 
fanya kelele sana, hawawezi kusikia sauti yako." 
Elisi akasikiliza na bila shaka paHkuwa na 
ghasia kubwa ndani; aHsikia kiHo cha mtoto 
mchanga, na chafya nyingi, na mara kwa mara 
shindo kubwa kana kwamba sahani au birika 
Hmevunjwavunjwa. EHsi akasema " Nataka 
kuingia." Chura akajibu " Mlango ungekuwa NGUBUWE NA PILIPILI 57 

kiziiio kati yetu ingefaa kupiga hodi." AK- 
pokuwa akisema Askari hakuacha kutazama 
mbinguni; Elisi akasema kimoyomoyo " Labda 
na lazima afanye hivi, maana macho yake ni 
juu ya kichwa chake, lakini sharti anijibu." 
Akapaza sauti akasema tena " Nataka kuingia." 
Chura akajibu ovyo akasema " Mimi nitakaa 
hapa mpaka kesho." Alipokuwa akisema mla- 
ngo ulifunguUwa na sahani kubwa (ihotupwa 
na mtu ndani ya nyumba) ikaruka ikampiga 
chura puani, ikavunjika penye shina la mti 
nyuma yake; Askari akaendelea kusema kana 
kwamba hakupigwa, akanena " . . . au labda 
kesho kutwa." Ehsi akajibu kwa hasira aka- 
sema, " Namna gani ! Nipe ruksa kuingia." 
Askari akanena " Je, umepewa ruksa kuingia 
na mwenye nyumba ?" Ehsi akanyamaza akao- 
na haya. Chura akaendelea kusema " Mimi 
nitakaa hapa mara kwa mara kwa siku nyingi 
sana." Ehsi akasema " Na mimi je ?" Aska- 
ri akapiga uruzi akasema " Fanya upendavyo." 
EHsi akasema kimoyomoyo " Hakuna faida 
kuzidi kusema naye, yeye mjinga kabisa." 
Akafungua mlango mwenyewe akaingia nyu- 
mbani. 

Ndani palikuwa na jiko la Kizungu; Hhlotoa 
moshi nyingi sana. Mama Mkubwa ahkuwa 
amekaa kitini akimbembeleza mtoto. Mpishi 
ahkuwa akikoroga chakula katika chungu kiku- 
bwa. EHsi akaenda chafya akasema " Zimo 58 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU Pilipili nyingi sana katika chakula!" Hata 
Mama Mkubwa alienda chafya mara kwa 
mara, na yule mtoto hakuacha kuenda 
chfaya na kulia. Walikuwa watu wawiH tu 
waliokuwa hawaendi chafya, walikuwa MpisM 
na Paka mkubwa aUyekuwa amekaa penye 
moto akichekelea sana. Elisi akasema " Shi- 
kamoo Mama Mkubwa. Tafadhah niambie kwa 
sababu gani Paka wako ametoa meno hivi ?" 
Mama Mkubwa akajibu akasema " Kwa saba- 
bu ni Paka Mcheshi. Nguruwe We !" AUse- 
ma maneno yale ya mwisho kwa nguvu sana, 
Ehsi akashtuka akadhani ya kuwa mama ame- NGURUWE NA PILIPILI 59 

msema yeye " Nguruwe " lakini alifahamu ya 
kuwa amemwita yule mtoto, akajipa moyo 
aksema " Sikujua ya kuwa paka huweza ku- 
chekelea !" Mama Mkubwa akajibu "Ana- 
weza. Tena wengi wametenda hivi." EUsi 
akanena " Mimi sijapata kuona paka ache- 
kaye," Mama Mkubwa akajibu " Pana mambo 
mengi ambao wewe hujapata kuona." Mpishi 
ahkiepua chungu jikoni, akatwaa vijiko na 
sufuria na sahani akawatupia Mama Mkubwa 
na mtoto, Mama hakumjaH mwanawe ambaye 
ahkuwa akilia sana wakati ule wote, wala 
haikujulikana kama amepigwa ama siyo. EUsi 
akasema " Angalia Mpishi wee umempiga mto- 
to !" Mama Mkubwa akasema " Watu wote 
wakishika lao uUmwengu utaendelea vizuri." 
Mpishi akarudi mekoni akakoroga chakula kwa 
nguvu, akazidi kunyunyiza pilipiH. Elisi aka- 
sema " TafadhaU Mama, niambie ..." Ma- 
ma Mkubwa akamkatiza maneno akasema " Usi- 
niudhi." Akambembeleza sana mtoto aka- 
mwimbia akisema: 

Mkaripie mwana wako, 
Na akienda chafya, 
Atenda hivi kusumbua, 
Hajambo, ana afya. 

Wote, pamoja na Mpisha na Mtoto Mchanga 
wakaitikia: " Wawawawawa " Mama akaimba 
ubeti wa pili, akamrusha mno mtoto, ahyelia 60 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

hata Elisi alisikia kwa shida maneno ya 
wimbo. 

Namkaripia mwana wangu, 
Nampiga akilia 
Apenda sana pilipili 
Na moshi chafu pia. 

Mama Mkubwa akamtupia Elisi mtoto mcha- 
nga akasema " Mshike wee, maana imenilazi- 
mu nijiweke tayari kucheza Kriketi na Malkia Key G minor. 
\ : I : n ) r : 


d 1 t, : i, 
se, : 1| 1 t, .t, :ri. 


M - ka 


ri - pi - e 
mwa-na wa-ko, Na 


{ d:l, 1 r:re 
a - ki - en - da 


i n : n, | 
chaf-ya, 
: n f : n 1 r : 1, 
A - ten-da hi - vi 


f ' 

\ n : r 1 d : S| 


1. : f 1 


n 


: 1, ! r :- 1 d :- 


ku-sum - bua, Ha 


- jam - bo. 


a - 


■ na af - - ya. Mzunguwapili." Akatoka chumbani, Mpishi 
akamtupia sufuria. 

EHsi aUmshika kwa shida mtoto, maana aH- 
kuwa ajinyonganyonga, mwisho akamshika sa- 
na kwa mguu wake wa kushoto na sikio la 
kulia, akamchukua nje mwituni apate kupu- 
nga hewa, akasema " Lazima nimpeleke nje, 
wasimwue kule jikoni. Pole mwanangu, wa 
mekupiga sana sivyo ? Watu hawa ni waji- 
nga kabisa, hawajui kukutunza." Mtoto aka- NGURUWE NA PILIPILI 61 " Usi- 
Yule guna kama kujibu, Elisi akamwambia 
gime ! Si vizuri kuguna kama nguruwe." 
Mtoto akazidi kuguna, Elisi akamtazama sana 
kwa mashaka, pua yake yalikuwa kama pua 
ya nguruwe, na macho yake yalikuwa madogo. 
Elisi akafikiri ya kuwa ni kwa sababu ya kulia 
sana ndipo akavimba pua; akaendelea kute- 
mbea akasema " Ukigeuka kabisa kuwa ngu- 
ruwe, basi wewe si mtoto wa kusuhubiana 
nawe." Mtoto akaguna tena, Elisi akatulia 
akamtazama kwa hofu, na ilikuwa hakuna 
shaka, mtoto alikuwa amekwisha geuka kuwa 
mtoto wa nguruwe. Ehsi akamsimamisha chi- 62 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

ni, akafurahai kumwona anaweza kutembea, 
alimtazama akikimbilia mwituni. 

Elisi, alipokuwa peke yake akainuisha ma- 
cho akashtuka kumwona Paka Mcheshi aUye- 
kuwa amekaa penye tawi la mti mbali kidogo. 
Ehsi akamsogelea Paka, naye ahkuwa ameche- 
kelea sana, yule mtoto akafikiri ya kwamba 
sura yake ihkuwa ya upole, lakini meno yake 
na kucha zake zilikuwa kah. Akasema kwa 
hofu kidogo " Hujambo Paka Mcheshi ?" " Wa- 
weza kunionyesha njia ?" Paka Mcheshi aka- 
jibu akasema " Wataka kwenda wapi ?" Ehsi 
akajibu " Po pote nitakapo !" 

" Kwa hiyo habari ya njia pia mamoja 
kwako." 

*' Afadhah nifike mahali pengine." 

" Ukienda mbah, bila shaka utafika pe- 
ngine !" 

" Watu gani wakaao hapa ?" 

Paka Mcheshi akaelekeza kwa mguu akasema 
" Huko amekaa Mwuza Kofia, na huko Kobe, 
nenda kamwamkie ye yote, wote wawih wana 
wazimu !" 

" Lakini mimi sipendi kusuhubiana na watu 
wenye kichaa." 

'' Kwako wewe mbwa ana akili ?" 

" Naam anayo akiH." 

" Vema, mbwa hutikisa mkia akipendezwa 
na kitu, hunguruma akikasirika, na mimi, 
nikikasirika natikisa mkia, nikifurai nanguru- 
shtuka kward siku ma, kwa hiyo najua 
sana ya kuwa mimi ni 
mwenye wazimu." 

" Lakini wewe hungu- 
rumi ! waguna tu." 

" Sema kama upe- 
ndavyo. Je, utakwenda 
Kriketi nk Malkia leo ?" 

" Ningependa sana 
kucheza, lakini sikui- 
twa." Paka Mcheshi 
akajibu akasema 
"Tutaonana tena 
huko." Akatoweka 
mara. Elisi haku- 
zile ahkuwa amekwisha zoea mambo ya namna hii, na aUpokuwa 64 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

akitazama mahali alipokuwapo paka yule 
mnyama akarudi tena akasema " Je, nini ha- 
bari za mtoto ? Nilisahau kukuuliza." Elisi 
akajibu akasema " Amegeuka nguruwe." Paka 
Mcheshi akacheka zaidi, akasema " Hii si 
ajabu kubwa." Akatoweka tena. Elisi aH- 
ngoja kidogo akifikiri ya kuwa labda atarudi, 
lakini hakumwona; akatembea kidogo katika 
njia aliyoionyeshwa na Paka Mcheshi, kufikia 
penye nyumba ya Mwuza Kofia. Kitambo 
kidogo akainuisha macho, akamwona tena Paka 
Mcheshi aliyekuwa amekaa katika tawi jingine, 
yule mnyama akasema " Uhsema ' Nguruwe ' 
au 'Ngurubai'?" Ehsi akajibu, "Nilisema 
' Nguruwe,' tena usitoweke upesi hivi, imenitia 
kizungukizungu." Paka Mcheshi akasema NGURUWE NA PILIPILI 65 " Vema !" Akaanza kutoweka pole pole, kwa- 
nza mkia, kisha mwili, halafu uso, na mwisho 
kinywa na kicheko; tena kinywa kilionekana 
kidogo baada ya kwisha kutoweka maungo 
yake. Elisi akasema " Haya ! Zamani ni- 
liona paka bila kicheko, bali sijapata kuona 
kicheko bila paka !" 

Kabla hajaenda mbali sana Elisi akaona 
nyumba ya Mwuza Kofia, ihkuwa nyumba 
kubwa, na hakuthubutu kuikaribia mpaka 
alipokwisha kula kidogo kipande cha uyoga 
cha mkono wa kushoto, aHchokifunga nguoni, 
ih apate kuongeza urefu kidogo. 

Urefu wake ukawa kama ule wa mtoto wa 
miaka miwih, akaikaribia nyumba, akasema 
" Naomba Mwuza Kofia awe hana kichaa sana." 
SURA VII 
KARAMU YA WENYE WAZIMU 

Palikuwa na meza chini ya mti, mbele ya 
nyumba; kwenye meza walikuwapo watu wa- 
tatu. Walikuwa: Kobe, Mwuza Kofia, na 
Komba. 

Komba alikuwa amelala usingizi na wenzake 
walimwagimia kwa visigino juu ya mgongo, 
walikuwa wakisema kwa kelele. Elisi akafikiri 
" Masikini Komba ! Lakini kwa kuwa amelala 
labda si vibaya." 

Ingawa meza ilikuwa kubwa watu wale 
watatu walikuwa wamekaa kwa kusongana 
sana penye pembe moja; na walipomwona KARAMU YA WENYE WAZIMU 67 

Elisi wote wakapaza sauti, wakisema pamoja 
" Hakuna nafasi, hakuna wasaa !" Elisi aka- 
jibu kwa hasira akasema " Kuna nafasi tele." 
Akakaa penye kiti kikubwa cha Eazungu. 
Kobe akasema " Wapenda kunywa mvinyo ?" 
Elisi akatazama mezani, hakuona kitu ila chai 
tu, akasema " Sioni mvinyo !" Kobe akajibu 
akasema " Hamna." Ehsi akasema " Basi si 
vizuri kuniitolea." Kobe akanywa chai aka- 
sema " Si vizuri kukaa penye meza yetu 
usipoitwa." EHsi akaona haya kidogo, lakini 
kwa kuwa amejua ya kwamba wenzake wali- 
kuwa wana wazimu akajipa moyo akajibu 
" Sikujua kama ni meza yenu, tena pana na- 
fasi ya watu wengi zaidi ya watatu." Mwuza 
Kofia akamtazama Elisi kwa makini akasema: 
" Nitamwita mzuzi, nywele zako si sawa sawa." 
Elisi akajibu " Shika lako. Huna adabu !" 
Mwuza Kofia akafumbua sana macho akasema 
" Je, Kwa nini kunguru amefanana na meza ?" 
EUsi akafurahai akasema " Haya ! Mafumbo ! 
Mimi najua maelezo yake." Kobe akasema 
" Wajua maana yake ?" Elisi akajibu " Ha- 
swa." Kobe akamwambia yule mtoto aka- 
sema " Sema kama uHvyonia." EHsi akajibu 
*' Kusema kama nilivyonia na kunia kama 
nilivyosema ni sawa sawa." Mwuza Kofia 
akafikiri sana akasema " Ni mbah mbah ka- 
bisa. Je, kuona ninachokula na kula nina- 
choona ni sawa sawa ? La !" Kobe akaitikia 68 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

akasema " Je, kupenda ninachopata, na kupata 
ninachopenda ni sawa sawa ? La !" Komba 
akafumbua macho akapaza sauti nyembamba 
akasema " Je, Kutoa pumzi nilalapo na kulala 
nitoapo pumzi ni sawa sawa ?" Mwuza Kofia 
akajibu akasema " Kwako wewe Komba si 
mbali, maana siku zote umelala." 

Wote wakanyamaza kidogo, Elisi akafikiri 
sana juu ya mafumbo ya kungura na meza, 
asielewe. Mwuza Kofia akasema " Leo ni siku 
gani ya mwezi ?" Alipokuwa akisema maneno 
haya akatoa saa mfukoni akaitazama sana, 
akaitetemesha akaiweka sikioni. Elisi aka- 
sema " Ni siku ya nne ya mwezi." Mwuza 
Kofia akamwambia Kobe akasema '* Saa hii 
imekosa majira kwa siku mbih. Nilikuambia 
ya kwambia siagi haifai kwa saa." Kobe 
akajibu kwa unyenyekevu akasema " Siagi 
ni nzuri sana." Mwuza Kofia akasema " Na- 
jua, lakini palikuwa na vipande vya mkate 
ndani yake, uhtia siagi kwa kisu cha kukatia 
mkate." Kobe akatwaa saa, akaitazama kwa 
huzuni akaichovya katika kikombe chake cha 
chai, akaitazama tena, akazidi kusema " Lakini 
ihkuwa siagi nzuri kabisa." Elisi pia ahita- 
zama saa, akasema kwa kustaajabu " Hii ni 
saa ya kabila gani ? Inaonyesha siku za mwezi 
tu ! Habari ya majira hakuna !" 

Mwuza Kofia akamwuHza Elisi akasema " Je, 
wewe unaya saa ya kuonyesha mwaka mzima ?" KARAMU YA WENYE WAZIMU 69 Elisi akajibu akasema " Saa za kuonyesha 
mwaka mzima hazipatikani maana mwaka 
mzima ni kipindi kikubwa." Mwuza Kofia 
akatazama mbinguni akafunga mikono aka- 
sema " Na mimi vile vile." EHsi hakufahamu 
akasema " Sielewi." Mwuza Kofia hakumjibu 
Elisi, akawa anamtazama Komba, ambaye 
amelala tena, akamwagia chai ya moto puani. 
Komba akajitetemesha akafumbua macho, aka- 
sema " Kweli ni kama uHvyosema." Mwuza 
Kofia akamwuliza EHsi akasema " Je, ume- 
kwisha fahamu majibu ya mafumbo ?" EHsi 
akajibu " Nimeshindwa kabisa, uniambie ma- 
jibu yake." Mwuza Kofia akapiga mwayo 
akasema " Mimi sijui hata kidogo." Kobe 70 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

akaitikia " Wala mimi sijui." Elisi akasema 
" Ni kupoteza nafasi kutoa mafumbo yasiyo- 
kuwa na majibu." Mwuza Kofia akashtuka 
akatetemeka akasema " Angalia mtoto ! Uli- 
pomjua ' Nafasi ' kama mimi nilivyomjua, 
ungalimtaja kwa heshima. Je, umepata ku- 
sema na Nafasi ?" Elisi akajibu " Sijapata 
kusema naye." Mwuza Kofia akajificha uso 
kwa mikono akasema " Mimi niligombana sana 
na Nafasi, zamani kidogo, wakati wa Machezo 
ya Malkia Mzunguwapili, nilipomwimbia . . . 
Ngoja ! Nitawaonyesheni wimbo niliouimba. 

Popo popo unang'aje ? 
Niambie wafanyaje ? 

Je, unajua wimbo huu ?" Elisi akajibu " Nu- 
jua kidogo kidogo." Mwuza Kofia akaendelea, 
akaimba hivi: 

" Kama buli, kama kuni 
Unaruka mbinguni. 

" Popo Popo unang'aaje ? 
Niambie wafanyaje. 
Popo Popo, niambie 
Wafanyaje ? 

Nimekuwa sijamahza ubeti wa pili ila Malkia 
akaondoka akapaza sauti sana akasema ' Amme- 
uawa Nafasi. Akatwe kichwa.' Na toka saa 
ile Nafasi ni adui yangu, sina bahati naye, KARAMU YA WENYE WAZIMTJ 71 

hanisaidii hata kidogo, na tangu saa ile siku 
zote ni saa kuini na moja." EHsi akacheka 
sana akasema " Sasa waeleza maana ya vyombo 
hivi vyingi mezani, vichache safi na vichache 
vichafu, kwa kuwa kila saa ni saa ya chakula 
cha jioni, na hakuna nafasi kuvisafisha." Mwu- 
za Kofia akajibu akasema " Haswa ! Hiyo 
ndiyo maana yake, nasi hatukai siku zote Key C. 

n:nln:l |se:l|n: — |d:r|n:l 

Po - po po - po u - nang'-aje ? Ni - am - bi - e 

se : 1 I d' : t | 1 : s | f : 1 | r' : d' | d' : 1 

wa - fan - ya - je. Ka-ma bu - li, ka - ma ku - ni 

f:l|r:n | f:l|l:s | d:rln:s 

U - na - ru - ka m-bing - u - ni. Po - po po-po 

d' : r I s :- I f : f I n : s | r : r | d :- 

u - nang'-aje ? Ni- am - bi - e Wa-fan - ya-je ? 

d : d I d' : d' | d : r | n : s | n : r | d :- | 

Po-po po-po, ni-am - bi-e Wa-fan-ya-je ? penye pembe hii ya meza, mara kwa mara 
tunazunguka mezani." Kobe akapiga mwayo 
akasema " TafadhaU Mama, tusimuHe hadi- 
thi." Ehsi akaogopa akasema " Mimi sijui 
hadithi." Kobe akasema " Vema. Ni juu ya 
Komba. Ewe ! Amka Kaka." Kobe na 
Mwuza Kofia wakamfinya sana. Komba aka- 
fumbua macho kwa pole pole, akasema kwa 72 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

sauti nyembamba " Mimi sikulala, nilisikia 
yote yaliyosemwa nanyi." Kobe akasema " Ve- 
ma. Tusimulie hadithi." Elisi akaitikia " Ha- 
ya, hadithi Bwana Komba." Mwuza Kofia 
akasema " Tena endelea upesi, usilale kabla 
hujamahza hadithi." Komba akasema kwa 
haraka " Hapo kale paHkuwa na watoto wa- 
tatu wanawake, majina yao yalikuwa ' Lusi, 
Lesi na Tih '; wote watatu wahkuwa wa- 
mekaa chini ya kisima." Ehsi akauliza kwa 
makini " Walikuwa wakila nini ?" Komba 
akafikiri kidogo akasema " Wamekula asali." 
EUsi akasema " Wangalikuwa wakila asah tu 
wangahkuwa hawawezi. Lakini kwa nini 
wahkuwa wamekaa chini ya kisima ?" Kobe 
akamwambia Ehsi akasema " Kunywa chai 
zaidi mwanangu." Ehsi akajibu akanena " Si- 
janywa chai baado, hata kidogo, kwa hiyo 
siwezi kunywa zaidi." Ehsi akatia chai katika 
kikombe akanywa, akauhza tena kwa nini 
watoto wale watatu wahkuwa wamekaa chini 
ya kisima. Komba akafikiri sana akajibu " Ki- 
hkuwa kisima chenye asah " Ehsi akasema 
kwa hasira " Hakuna kisima chenye asah." 
Komba akasema " Kama huwezi kuwa na 
adabu afadhah uendelee wewe na hadithi. 
Ehsi akajibu kwa unyenyekevu akasema Nasi- 
kitika Bwana Komba, tafadhah endelea na 
hadithi, sitakatiza tena maneno yako, labda 
hupatikana kisima cha asah." Komba aka- KARAMTJ YA WENYE WAZIMU 73 vuta pumzi akaendelea akasema " Watoto wa- 
tatu walikuwa wakijifunza kuteka "... Elisi 
alisahau ahadi yake aliyoitoa, akasema " Ku- 
teka nini ?" Komba akajibu kwa uvumilivu 
akasema " Waliteka asali." Mwuza Kofia aka- 
sema " Nataka kikombe safi, wote wabadili 
viti." Wote wakasogea kulia, lakini Mwuza 
Kofia peke yake ndiye aliyepata faida, maana 
wengine walikuwa wamekaa katika viti vya 
wenzao. Elisi alikuwa amekaa katika kiti cha 
Kobe; sehemu yake ya meza haikuwa safi. 
EHsi hakutaka kumsumbua tena Komba, aka- 
sema kwa sauti ndogo " Lakini sijafahamu, 
wameteka asali katika nini ?" Mwuza Kofia 
akasema " Mjinga we ! Waweza kuteka maji 
katika kisima cha maji, na waweza kuteka 
asali katika kisima cha asali." Elisi hakuu- 74 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

dhiki akasema " Lakini komba alisema ya 
kuwa watoto wenyewe walikuwamo kisimani." 
Komba akasema " kweli, walikuwamo, tena 
walikuwa wakijifunza kuandika herufi ' M.' " 
Elisi akauHza " Kwa nini ' M ' tu ?" Kobe 
akajibu " Maana ' M ' ni herufi nzuri." Elisi 
akanyamaza, " Komba akafumba macho aka- 
lala usingizi." Kobe na Mwuza Kofia wa- 
kamfinya, akaamka mara akaitikia " Herufi 
' M.' " EHsi alikuwa amechoka na upumbafu 
huu, akaondoka, akawaaga wengine akaenda 
zake, Komba akazidi kulala. Alipokuwa mba- 
li kidogo Elisi ahgeuka akamwona Kobe na 
Mwuza Kofia wakimtia Komba buhni. Yule 
mtoto akasema " Paka Mcheshi alisema kweh, 
wote wawiH ni wana wazimu. Sitarudi kwao. 
Sijapata kuona karamu ya ujinga kupita hii." 
Kabla hajamaliza maneno haya akaona shina 
la mti mkubwa lenye mlango; akaingia na 
kumbe, aHjiona katika kile chumba kirefu 
chenye milango mingi, akafurahai sana aka- 
sema " Sasa naweza kuingia bustanini, lakini 
lazima nisisahau ufunguo." Akautwaa katika 
ile meza ya kioo, akaufungua ule mlango 
mdogo, akala kidogo kipande cha uyoga mpaka 
urefu wake ukawa kama ule wa kuku, akaingia 
pangoni, na mwisho akafika kwenye bustani 
nzuri yenye maua ya kila rangi na chemchemi 
ya maji baridi. 
^^w ^^^^^^^^J^^ SURA VIII 

MACHEZO YA IMALKIA 

Alipoingia bustanini Elisi aliona mti wa ma- 
waridi, wenye maua meupe, lakini watunzaji 
bustani watatu walikuwa wakiyatia rangi nye- 
kundu. Elisi akakaribia kidogo, apate kuona 
vizuri kazi yao, akasikiliza mazungumzo, Mtu 
mmoja akasema " Sasa angalia Tano, usini- 
mwagie dawa hivi." Tano akajibu kwa hasira 
akasema " Si kosa langu, Saba alinipiga kisi- 
gino." Saba akajibu kwa kiburi akasema 
" Ni desturi yako kushtaki watu siku zote." 
Tano akajibu " Wewe huwezi kujisifu, juzi 

75 76 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

nilimsikia Malkia akisema kuwa wastahili kuka- 
twa kichwa." Mtunzaji wa kwanza akauHza 
" Kwa sababu gani ?" Saba akajibu " Nita- 
mwambia Tano. Sababu ilikuwa hii: Saba 
alimpelekea Mpishi viazi aUpotumwa vitu- 
nguu." Saba akaangusha burashi yake ya 
kupakia rangi akasema kwa uhasidi " Sikusa- 
diki, maneno yako ..." Kwa ghafula yule 
Mtunzaji alimwona Elisi, akajikatiza maneno, 
akamsalamia sana, wengine wakamwamkia pa- 
moja. Ehsi akawauliza kwa makini akasema 
" Niambie, ni kwa nini mmeyatia rangi maua ?" 
Tano na Saba wakanyamaza, wakamtazama 
Mbili, ambaye alikuwa akisema " Malkia ali- 
tuamuru kupanda miti ya mawaridi yenye 
maua mekundu, nasi tuHkosa tukapanda miti 
yenye maua meupe, na sasa tunapaka maua 
rangi hiyo, makusudi kumdanganya Malkia, 
asitukate kichwa." Ahpokuwa akisema neno 
la mwisho Mtunzaji Tano akapiga yowe aka- 
sema " Tazameni ! Malkia MzunguwapiH ! 
Malkia Mzunguwapili ! Amekuja." Watunza- 
ji bustani wakaanguka wote watatu wakalala 
kifudifudi, EHsi akasikia sauti nyingi kwa mbaH 
kidogo, akageuka, apate kumwona Malkia. 

Watu wengi waHkuwa wakifuatana kwa safu. 
Kwanza Askari kumi wenye rungu. (Askari ha- 
wa wamefanana na Watunzaji bustani isipo- 
kuwa mavazi yao, miili yao yaHkuwa miraba 
batabata, miguu yao imetokeza pembeni cha MACHEZO YA MALIvIA 77 cliini, na mikono imetokeza pembeni kwa 
juu.) 

Kisha katika mfuatano wakapita Mawakili 
kumi, wamepambwa kwa alama ya Huru Ka- 
rata, wakaenda wawili wawili kiaskari, halafu 
wakaja watoto wa Mfalme Mzunguwanne ku- 78 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

mi, walikuwa wameshikiana mikono, wote wa- 
mepambwa alama ya kopa. Mwisho wakaja 
wageni, wote wafalme na malkia, na pamoja na 
hawa EHsi ahmwona Sungura Mweupe aHye- 
kuwa amesemasema sana; lakini yeye haku- 
mwona Elisi akampita. Mzunguwatatu, Mja- 
nja wa Kopa akawatanguHa Mfalme Mzungu- 
wanne na Malkia MzunguwapiH wa Kopa, naye 
aHkuwa amechukua taji iHyowekwa juu ya 
takia, na mwisho kabisa wa maandamano ha- 
ya maarufu wakaja Mfalme Mzunguwanne na 
Malkia MzunguwapiH wa Kopa wenyewe. 

EHsi akaona shaka kidogo akafikiri ya kwa- 
mba labda iHkuwa desturi ya nchi ile ya ajabu, 
kulala kifudifudi mbele ya Mfalme na Malkia 
kama waHvyolala Watunzaji bustani, lakini 
aHtaka sana kuyatazama mavazi ya umaHdadi 
na utukufu wa wakuu hawa, kwa hiyo aHsi- 
mama kimya akangoja. 

WaHpokuwa wamemkaribia EHsi, watu wote 
wakatuHa, MaUiia akamwelekeza kidole, aka- 
mwuHza Mjanja Mzunguwatatu akasema " Na- 
ni huyu ?" Mjanja akasimama mbele ya Ma- 
Ikia akacheka akanyamaza. Malkia akasita, 
akasema kwa hasira " Mpumbafu we !" Aka- 
mwuHza EHsi mwenyewe akasema " Jina lako 
nani mwanangu ?" EHsi akajibu " Jina langu 
EHsi." Akafikiri akasema kimoyomoyo " Ha- 
ya ! Hawa wote ni watu wa karata tu, si- 
waogopi." MACHEZO YA MALKIA 79 

Malkia akawaona wale Watunzaji bustani 
watatu, hata wakate ule walikuwa wamelala 
kifudifudi, akawatazama akauliza " Nani ha- 
wa ?" (Wafahanu Msomaji ya kuwa migongo 
yote ya Karata imefanana, na kwa hiyo Malkia 
ahkuwa hakujua wa nani. Hakuweza kuwa- 
tambua kuwa waUkuwa askari au mawakili 
au watoto wake mwenyewe.) 

EHsi akajibu " Mimi sijui. Mimi nashika 
langu." Malkia akatetemeka kwa hasira aka- 
mtazama EHsi kama mnyama ya mwitu, mwe- 
nye macho ya kung'aa, akapaza sauti akasema 
" Mkate kichwa ! Mkate Klchwa ! Mk . . ." 
Ehsi akamkatiza maneno akasema " La ! Ha- 
pana ! Upumbafu gani huu ?" Malkia aka- 
tulia, Mfalme akamgusa mkono akamwambia 
" Fikiri Mpenzi, huyu ni mtoto tu." Malkia 
akageuka kwa haraka akamwambia Mjanja 
" Wageuze hawa." Mjanja akazigeuza zile 
karata tatu kwa mguu. Malkia akatoa sauti 
kuu akasema " Simameni." Watunzaji wa- 
kaondoka mara, wakaanza kumsujudia sana. 
Malkia akasema " Tulieni, mnanitia kizungu- 
zungu." Malkia akautazama ule mti wa ma- 
waridi akasema " Mmefanyaje hapa ?" Mbili 
akapiga magoti akasema " Shikamoo Malkia 
mtukufu, Tusamehe; tumejaribu . . . ." Ma- 
Ikia akamkatiza maneno akasema " Naona 
maua, ► nafahamu sana. Wakate kichwa !" 
Watu wengine wakaendelea kuandamana ih- 80 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

kuwa imebaki Watunzaji bustani watatu, na 
askari watatu na Elisi. 

Watunzaji wakamkimbilia Elisi wapate ku- 
hifadhiwa naye. Ehsi akawafariji akasema 
" Nawapeni pole, hamtuuawa nanyi kamwe." 
Akawaficha kwa upesi katika mtungi mkubwa 
uliokuwapo karibu. Askari wakawatafuta 
Watunzaji muda wa dakika chache, halafu 
wakakata tamaa wakawafuata wenzao. Malkia 
akapiga kelele akasema " Wamekatwa ki- 
chwa ?" Askari wakajibu " Vichwa vyao ha- 
vionekani." Malkia akasema " Vema." Ehsi 
akakaribia. Malkia akamwuhza Askari aka- 
sema " Huyu ajua kucheza Kriketi ?" Askari 
akanyamaza. Ehsi akajibu mwenyewe aka- 
sema " Ndio, najua kucheza." Malkia akasema 
kwa sauti kah " Twendeni !" Wote wakaende- 
lea kuandamana; Ehsi pia ahjiona akitembea 
pamoja na Sungura Mweupe, ambaye ahsema 
" Jua kah sana leo siyo ?" Ehsi akajibu 
" Kweh ni kah. Je, umemwona Mama Mku- 
bwa ?" Sungura akajibu " Nyamaza mwana- 
ngu," akamtazama kwa hofu Malkia ahye- 
kuwa akitembea nyuma yake, akachuchumia 
akamnong'oneza Ehsi akasema " Kesho Mama 
Mkubwa atakatwa kichwa." Ehsi akasema 
" Amekosa nini ?" Sunguru akamwuhza 
" Unamwonea huruma ?" Ehsi akamwambia 
" La. Ni mtu mbaya, astahih kukatwa ki- 
chwa, nihkuuhza amekosa nini ?" Sungura MACHEZO YA MALKIA 81 akasema " Amempiga kofi Malkia." Elisi aka- 
cheka sana, Sungura akatetemeka kwa hofu 
akasema " Angaha, Malkia atakusikia; Mama 
Mkubwa ahkuwa amechelewa kidogo, na Ma- 
Ikia amemkaripia, na . . ." Malkia akamka- 
tiza maneno, akapiga kelele akasema " Kila 
mtu aende mahaii pake." Wote wakapiga 
mbio, wakaenda ovyo kabisa, wakasimama 
huko na huko, wakaanza kucheza. Ndiyo 
kwanza EHsi aone kiwanja cha Kriketi cha 
namna hiyo, kiUkuwa matuta matupu. Badala 
ya kibau cha kupigia mpira wahtumia korongo 82 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

mwekundu, na mpira wenyewe ulikuwa kaka- 
kuona, na vijiti vilikuwa askari watatu walio- 
kuwa wamesimama pamoja. 

Wakati wa zamu ya Elisi ya kupiga mpira 
aliona taabu kidogo kwa sababu ya korongo, 
alimshika kiwiliwili, na miguu yake ilikuwa 
inaning'inia nyuma; lakini kila mara akimnyo- 
sha shingo, yeye huikunja, kumtazama usoni, 
na Elisi ahkuwa sharti aeheke, tena mara kwa 
mara ule mpira kakakuona uHtembeatembea. 

Wachezaji walikuwa hucheza wote pamoja, 
hawakungojea kwa zamu, wote hugombana na 
Malkia aUkuwa amekasirika sana, aHpiga kelele 
akajisemea ovyo mara mbili tatu kila dakika 
" Mkate kichwa ! Mkate kichwa !" Ehsi aka- 
ona shaka akasema kimoyomoyo. " Akiendelea 
hivi, halafu watakuwa wamekatwa kichwa wo- 
te, labda hata mimi pia !" Ehsi akatafuta njia 
ya kutoroka bila kufanya matata, na ahpokuwa 
akitafuta akaona wingu mbinguni, akahtazama 
sana, akaona winguni meno na kinywa chenye 
kutabusamu, akafurahi akasema moyoni "Ha- 
ya ! Yule Paka Mcheshi. Sasa nitakuwa na 
rafiki." Kinjrwa chake kilipotosha kusema 
Paka Mcheshi akamwambia Ehsi akasema " Wa- 
onaje mwanangu ?" Ehsi akangoja mpaka 
masikio yake yahkuwa yameonekana, akasema 
kimoyomoyo " Si vizuri kumjibu mpaka masi- 
kio yake yameonekana pia." Ahkuwa haku- 
ngoja sana ila kichwa chote kihonekana; Paka MACHEZO YA MALKIA 83 

akafikiri ya kwamba kichwa kitatosha, kwa 
hiyo hapana haja ya maungo yake kuonekana 
EUsi akasema " Hujambo Paka Mcheshi ? 
Watu hawa hawachezi sawasawa, tena wamego 
mbana sana, na kanuni za machezo hawazifu 
ati." Paka akauHza " Je, unampenda Malkia ?' 
EUsi akajibu " Simpendi hata kidogo . . .' 
Akajikatiza maneno kwa haraka, kwa kuwa 
Malkia mwenyewe aUkuwa amesimama karibu 
naye, akaendelea kusema kwa hila akasema 
" Kwa sababu amecheza vizuri sana, wote 
hawana bahati ila yeye." Malkia akacheka 
akaenda zake. 

Mfalme akamkaribia EUsi akakitazama kile 
kichwa cha Paka; akamwuUza EUsi akasema 
" Dude gani hiU ?" EUsi akajibu " Ni rafiki 
yangu Bwana Paka Mcheshi." Mfalme akane- 
na " Simpendi hata kidogo ! Lakini, akipenda, 
ana ruksa ya kunibusu mkono." Paka Mche- 
shi akajibu " Sipendi." Mfalme akakasirika 
akasema "Usinitolee ujuvi !" akajificha nyuma 
yake EUsi, akasema "Naogopa." EUsi akajibu 
kwa kumfariji akasema " Paka ana ruksa ku- 
mtazama Mfalme. Nimesoma maneno haya 
kitabuni." Mfalme akasema " Lazima aondo- 
lewe." Akamwita Malkia akamwambia " Wa- 
mwona Paka yule ? Lazima aondolewe." Ma- 
Ikia hakujua njia yo yote kuwahamisha adui 
zake isipokuwa kuamuru wakatwe kichwa, kwa 
hiyo akasema " Mkate kichwa." Mfalme aka- 84 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU sema " Nitamtafuta Askari mwenyewe." Aka- 
enda zake kwa haraka. 

Elisi akarudi kiwanjani apate kuwaona wali- 
oshinda, lakini wote walikuwa wameendeiea 
kucheza kwa wasi wasi, na wachezaji watatu 
walikuwa wamekwisha wekwa gerezani. Elisi 
akageuka akaona ya kwamba kundi kubwa 
la watu linamzunguka Paka; nalo hUkuwa liki- 
fanya shauri ya kumkamata kichwa; wote MACHEZO YA MALKIA 85 

wakawa wanasema pamoja, wakafanya kelele 
sana. 

Alipomwona Elisi, Malkia akamwita aka- 
mwumuru yeye kufanya shauri. Shauri la 
Askari lilikuwa: " Haiwezekani kumkata ki- 
chwa mtu asiyekuwa na mwili." Shauri la 
Mfahne liMkuwa: " Kila mtu mwenye kichwa 
aweza kukatwa kichwa." Shauri la Malkia 
hHkuwa: " Kazi hii isipotimizwa upesi watu 
wote watakatwa kichwa." 

EHsi akafikiri kidogo akesama " Paka Mche- 
shi ni mah ya Mama Mkubwa, afadhaU aitwe." 
Malkia akasema " Amefungwa gerezani, mlete 
hapa sasa hivi." Askari akaenda mbio na ufu- 
nguo mkubwa wa gereza. Kichwa cha Paka 
Mcheshi kihanza kutoweka. Basi Mfalme na 
askari wakakimbia huko na huko wakakita- 
futa, na wengine wakarudi kiwanjani. SURA IX 

HADITHI YA KASA 

Mama Mkubwa alimsalimia Elisi akasema 
" Nafurahi sana kuonana nawe mwanangu." 
Elisi pia akafurahi kuona ya kwamba Mama 
Mkubwa alikuwa mwenye hah njema, akafikiri 
ya kuwa labda hasira yake jikoni ilikuwa kwa 
sababu ya piHpili tu, akasema kimoyomoyo 
" Nitakapokuwa mama mkubwa mimi, sita- 
kula pihpiU hata kidogo, chakula bila pilipili 
si kibaya; labda pilipili ni sababu ya hasira 
yote duniani, mtu akila pilipiH huwa na hasira, 
basi angekula kwinini angekuwa mchungu, na 
angekula sukari angekuwa tamu." 

Kwa sababu ya mawazo yake Elisi alimsa- 
hau Mama Mkubwa, ambaye alikuwa ame- 
fuatana naye, akashtuka aUposika sauti yake. 
Mama Mkubwa akasema " Unafikiri sana mwa- 
nangu, kwa hiyo unasahau kusema; sasa hivi 
siwezi kukumbuka fundisho la maneno haya, 
lakini nitakumbuka bado kidogo." EHsi aka- 
jibu " Labda hahna fundisho !" Mama Mku- 
bwa akasema " Hasha ! Mwanangu, mambo 
yote yana mafundisho kama ungeweza kuya- 
fahamu." Alipokuwa katika kusema ma- 

86 HADITHI YA KASA 87 

neno haya akamjongelea sana Elisi, akamwekea 
kidevu katika bega lake, kijana hakupendezwa 
na tendo hili hata kidogo lakini hakutaka ku- 
mkataza, akasema " Sasa wanacheza kwa uta- 
ratibu." Mama Mkubwa akajibu " Kweli mwa- 
nangu, na fundisho lililokuambia ndilo: ' Elimu 
ndio mwanga yongozayo kila shani.' " EHsi 
akacheka akasema " Nikukumbushe Mama ya 
kuwa zamani kidogo ulisema ya kwamba uU- 
mwengu umeendeshwa na watu waHoshika 
yao." Mama Mkubwa akasema " Tofauti ba- 
ina ya kushika lako na Elimu si kubwa, na mi- 
mi nitapenda sana kukushika mkono, lakini 
naogopa korongo wako, nadhani ana haU mba- 
ya, je, nijaribu ?" Elisi akajibu akasema 
" Labda atakuuma." Alisema kivi kwa saba- 
bu hakutaka kushikiana mikono na Mama 
Mkubwa; huyu akasema " Kweli korongo ni 
ndege mkali — ^kama haradaH, vyote viwiH hu- 
uma, na f undisho lake ndilo : ' Ndege wa 
kabila moja huruka pamoja.' " EHsi akasema 
" Lakini haradaH si ndege !" Mama Mkubwa 
akajibu " Bila shaka haradaH ni madini, pana 
shimo kubwa la haradaH, wala si mbaH sana 
na hapa, na fundisho lake ndilo hiH: ' Paka 
akiondoka, panya hutawala.' " EHsi haku- 
jibu. Mama Mkubwa akasema " Unazidi kufi- 
kiri ?" EHsi akajibu kwa kuudhika " Lazima 
nifikiri " Mama akajibu kwa dharau akasema 
*' Imekulazimu kufikiri kama iHvyomlazimisha 88 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU nguruwe kuruka hewani, na mafundisho . . ." 
Wazungumzaji nawa wakamwona Malkia Mzu- 
nguwapili ambaye aUkuwa amesimama mbele 
yao, wote wawiH wakashtuka sana, Malkia 
amejikumbata mwenye sura mbaya kwa ha- 
sira. Mama Mkubwa akatetemeka kwa hofu, 
hata hakuweza kuwapasha wenzake habari za 
fundisho la maneno yake. 

Malkia alimtazama Mama Mkubwa kwa chu- 
ki; Mama ahmsalimu sana, akasema kwa sauti 
ndogo " Shikamoo Bibi." Malkia hakuitikia, HADITHI YA KASA 89 

akapiga meno aksema " Nimekuonya sana, 
Mama Mkubwa, na sasa chagua. Wewe uende 
zako au kichwa chako kiende zake." Mama 
Mkubwa hakukawia kuchagua, akapandisha 
nguo akakimbia upesi. Malkia akamwambia 
EHsi akasema '' Twende tukaendelee kucheza." 
EHsi hakuthubutu kukataa, akamfuata Malkia, 
wote wawili wakafudi kiwanjani. 

Wageni wengine waHkuwa wakipumzika ki- 
vuHni, iakini waHpomwona Malkia waHondoka 
mara wakaenda mahaH pao, wakaendelea ku- 
cheza kwa haraka, wakacheza muda wa saa 
nzima, na Malkia hakukoma kugombana na 
wenzake, na kuamuru fulani na fuiani akatwe 
kichwa, mpaka wageni wote wakaondolewa, 
hakubaki mtu kiwanjani ila Mfalme na MaUiia 
na EHsi. 

Malkia akawa amechoka sana, akawa ana- 
tweta, akamwambia Elisi " Je, umemwona 
Bwana Kasa MHaji"? EHsi akajibu " Siku- 
mwona." Malkia aksema " Vema. Twende 
tukamwamkie ! Tena ataweza kukuhadithia 
habari za maisha yake." WaHpokuwa waki- 
tembea pamoja EHsi akamsikia Mfalme Mzu- 
nguwanne mbaH kidogo, akiwaambia wageni 
kuwa wamekwisha samehewa. Mtoto akafu- 
rahi sana. 

Malkia na EHsi wakazunguka pembe ya 
njia, wakakutana na Mbuzi, aHkuwa amelala 
Uvsingizi. Malkia akampiga Mbuzi akamwa- 90 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

mbia " Ondoka mvivu we, mpeleke mtoto 
huyu kwa Bwana Kasa Mliaji, apate kusikia 
hadithi yake. Mimi lazima nirudi. Wageni 
wote watakatwa kichwa." Akaenda zake, aka- 
waacha Elisi na Mbuzi pamoja peke yao. 
Ehsi hakupenda sana sura ya Mbuzi yule, 
lakini kutofautisha baina ya ukaH wa Malkia 
na ukaH wa Mbuzi ilikuwa kazi ngumu. 

Mbuzi alimtazama yule mtoto kwa makini 
muda wa dakika chache halafu akageuka aka- 
mtazama Malkia ambaye alikuwa akienda, 
akasema " Kicheko kiko huko !" EHsi akau- 
hza " Kicheko gani ?" Mbuzi akajibu akasema 
" Malkia anadhani ya kuwa wageni wote wa- 
tauawa, lakini sivyo, hawatakatwa kichwa, 
hata mmoja ! Twende !" Mbuzi akaondoka 
EHsi akamfuata. Kabla hawajaenda mbaH 
wakamwona Kasa Mliaji; aHkuwa amekaa peke 
yake penye mwamba mkubwa, akiHa sana 
akitoa machozi. Bahari iHkuwa nyuma yake, 
na bahari ile iHkuwa machozi yake aHyoyatoa 
tangu zamani sana. EHsi akamwuHza Mbuzi 
akasema " Je, amefiwa, ana huzuni gani ?" 
Mbuzi akajibu " Hana huzuni, wala hakufiwa, 
kama ungemwuHza sababu ya msiba wake 
asingeweza kujibu, ametumwa na MaUda ku- 
jaza bahari watoto wake wapate kuogelea 
ndani." 

WaHpomkaribia Kasa MHaji, Mbuzi akamsa- 
Umia akasema " Shikamoo Kasa MHaji." Kasa HADITHI YA KASA 91 akafumbua macho na yakatoka machozi me- 
ngi sana, yanayotosha kujaza ndoo mbili, 
EHsi akarudi upesi asiingie maji. Kasa Mliaji 
akasema kwa shida " Marahaba. Wataka nini 
rafiki yangu ?" Mbuzi akajibu " Tafadhali 
mhadithie mtoto huyu habari za maisha yako." 92 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

Kasa Mliaji akatoa machozi zaidi akasema 
" Vema. Kaeni. Tena msinitietie mpaka ni- 
takapokuwa nimekwisha kusema." Wote wa- 
kakaa kitako, wakanyamaza muda wa dakika 
chache. EHsi akasema kimoyomoyo " Asi- 
ngeanza kusema angekuwa hawezi kuisha !" 
Akangoja kwa uvumilivu. Kasa MHaji aka- 
vuta pumzi akasema: 

" Hapo kale mimi na ndugu zangu tulikuwa 
tumekaa baharini, sisi sote tumehudhuria shule. 
MwaHmu wetu ahkuwa mzee." Tulimwita 
"ruNDi." EHsi akauhza "Kwa nini uHmwita 
' Fundi ' ?" Kasa akajibu akasema " KweH 
wewe mpumbafu ! Tumemwita ' fundi ' maa- 
na aHtuFUNDisha." Mbuzi akasema " EHsi 
mwanangu, sikujua kuwa wewe u mjinga kama 
hivi!" EHsi akaona aibu akanyamaza. Mbuzi 
akamwambia Kasa akasema " Endelea Kaka, 
sisi hatutaki kukaa hapa mpaka usiku." Kasa 
Mliaji akaendelea akasema " Sisi tuHfundishwa 
vizuri, tena tumekwenda kila siku chuoni." 
EHsi akamkatiza maneno akasema " Usiwe na 
kiburi Bwana Kasa, mimi pia nakwenda kila 
siku chuoni." Kasa MHaji akauHza " Ume- 
fundishwa kigha na ngoma ?" EHsi akajibu 
" Najifunza kuandika na kusoma." Kasa 
akaitikia " Kwetu sisi tuHfundishwa kukandika 
na kuchoma, halafu namna mbaHmbaH ya 
Hesabu, ndizo: Haki, Kudanganya, Kubudi- 
sha, na Karamu." EHsi akasema " Maneno HADITHI YA KASA 93 yako ni kama mafumbo ! Habari za masomo 
mengine ?" Kasa Mliaji akasema " Tumesoma 
' Kiburi cha thamani ' (Habari za zamani)." 
Mbuzi akasema " Basi Kasa ! Sasa tuambie 
kidogo habari ya machezo ya shule." '^-^^ 
SURA X 

NGOMA YA KAMBA 

Kasa akamwambia Elisi akasema " Wewe je, 
umepata kukaa chini ya bahari ?" EHsi aka- 
jibu " Sijapata kufika huko hata siku moja/' 
Kasa akanena " Wawajua sana Kamba ?" 
Elisi akajibu akasema " Mara moja niHwao- 

nj !" Akajikatiza maneno upesi, akasema 

'* Siwajui," Kasa akajibu " Kwa hiyo huwezi 
kujua furaha ya ngoma ya Kamba ?" EUsi 
akauliza " Ni ngoma ya namna gani ?" Mbuzi 
akaeleza akasema " Kwanza Kamba huenda 
pwani, tena kushikiana mikono halafu wote 
huogelea baharini na kurudi." Ehsi akataba- 
samu akasema " Ngoma nzuri sana !" Kasa 
akaondoka akasema " Twende. Tutakuonye- 
sha. Wanyama wawiH wakasimama, wakashi- 
kiana mikono wakaanza kuchezacheza katika 
mchanga." Wakamtisha sana Ehsi, mana 
miguu yao iUkuwa mikubwa, tena waHkuwa 
hawachezi sawasawa. IHkuwa hakuna ngoma 
lakini Kasa MHaji aHimba kwa upole na hu- 
zuni; Hivi: 

94 NGOMA YA KAMBA 96 

Key Ei? 

{| — : s.f I n.,n : s.s | d'.d, : s .s | n.n : s.s 
Che-wa a-mwa-mbia Ko-a, Ta-fa - dha-li ka-sa 

{ I d'. d' : s. f I n .n : s .s | d' .d' : d' .d' | t .s : 1 .r 
mwen-do, Nyu-ma yan-gu Pa-pa mku-bwa, ni-a ya-ke si ya 

I s . s : - .8 I 1 .1 : r' .r' | s .s : d' .d' 
pen-do, Ta - za-ma ka-ma Kam-ba wo-te 

I f .f : t .1 I s : 1 .Pi I s .f : s .r | f .n : r .d 
wa-me-tan-gu - lia, Wo-te wa-na-che-za pwa-ni, na n- 

I n .n : r .d | r : s .,s | n .n : s .s | d' .d' : s .s 
go-ma na-si - ki - a. Wa - we-za che-za 'we-za che-za 

I n .n : s .s | d' : s | n .,n : s .s | d' .d' : s .n 
'we-za che-za na - si, 'we-za che-za 'we-za che-za f .1 : s .s I s : — .s 
'we-za che-za na - - si . s Chewa amwambia Koa, " Tafadhali kaza 

mwendo, 
Nyuma yangu Papa mkubwa, nia yake si ya 

pendo, 
Tazama kama Kamba wote wametanguUa, 
Wote wanacheza pwani, na ngoma nasikia. 

Waweza cheza 'weza cheza 'weza cheza nasi. 
Waweza cheza 'weza cheza 'weza cheza 
nasi. 

Tukitupwa baharini tutaogelea sana," 

Koa akatetemeka, akasema '' La ! Hapana. 96 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

Itakuwa mbali mno, tena haiwezekani, 
Nenda peke yako Chewa, nitakungoja pwani. 

Siwezi cheza 'wezi cheza 'wezi cheza nanyi 
Siwezi cheza 'wezi cheza 'wezi cheza nanyi." 

Samaki akasema " Pana pwani mpya ng'a- 

mbo, 
Haya ! Jipe moyo Koa, sisi sote hatuja- 

mbo; 
Mbah na Afrika ni karibu Bara Hindi 
Njoo, kacheza Koa, usipige we mapindi. 

Waweza cheza 'weza cheza 'weza cheza nasi, 
Waweza cheza 'weza cheza 'weza cheza 
nasi." 

Wahpokuwa wamekwisha kucheza EHsi aka- 
washukuru akasema " Asanti sana rafiki zangu, 
na sasa mmechoka, kaeni, na mimi nitawaha- 
dithieni matokeo ya leo, tangu asubuhi. Jana 
nilikuwa mtoto mwingine, kwa hiyo ni bora 
nianze hadithi yangu tokea alfajiri leo." EHsi 
akasimuha matokeo yake, toka ahpomfuata 
Sungura Mweupe katika pango lake na mpaka 
mwisho. Ahpokuwa akihadithia jinsi ahvyo- 
mtiisha Mdudu kwa kusoma shairi, Kasa aka- 
vuta pumzi akasema " Haya ni mambo ya 
ajabu. Sasa jaribu tena kusoma mashairi. 
Simama. Funga mikono nyuma. Useme shai- NGOMA YA KAMBA 97 

ri la ' Ni sauti ya mvivu ' na beti zifuatazo.' 
Elisi akasema kimoyomoyo " Viumbe hawa 
wanitiishe ! Ni kana kwamba niko chuoni !' 
Akaondoka akafunga mikono akasoma: 

Key F. 
{|s:s:s|n:n:n|f:f:f|r :r :r.r|n:n:nid:d:d 
Ni-na-si-ki-a sa-u-ti ya Kam-ba " Ni-me-pi-kwa za-i-di, ta- 

•Jl r : r :r I t| :t| : t| I d :d :d ! 1, :1, : 1, | r :r :r | s, :s, :Si .s, 
-za-ma ma-gamba! Me-kun-du ka-bi-sa! 'si-ka-e mi-le-le, Ni-on 

-J I 1, :t| :d I t, :d :r I n :f :s I s : s : 1 1 1 :t :t 1 s : s : s 
-do-ke ka-ti-a su-ka-ri ny-we-le." Ka-ti-ka m-cha-nga naam 

{ I 1 :1 :1 I fe :fe :fe I s : s : s 1 n :n :n | f : f : f j r : r : r 
a-li-ji-ta-pa, Na A-ki-dha-ra-u ma - ta-ya ya Pa-pa. La- 

■jl n :n :n 1 d :d :d | r :5r :r | t, :- :t, 
- ki-ni wa - ka - ti wa ma-ji ma - ku - - u 

{| d :d :d 1 1, :1, :i, I t, :1, :t, I n, :- :- | 
A - li - sa - ha - u u - ho - da - ri huu. 

Ninasikia sauti ya Kamba 
" Nimepikwa zaidi, tazama magamba ! 
Mekundu kabisa ! 'sikae milele, 
Niondoke katia sukari nywele." 

Katika mchanga naam ahjitapa, 
Na akidharau mataya ya Papa. 
Lakini wakati wa maji makuu 
AHsahau uhodari huu. 

7 

AIW G 98 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

Mbuzi akasema '' Nilipokuwa mtoto mimi nili- 
jifunza kusoma maneno haya, kwa moyo, bali 
wewe umeyasoma vibaya !" Elisi hakujibu, 
akajikumbata akatazama bahari akafikiri sana 
juu ya matendo yake, na usahaulivu wake. 
Alikuwa amefadhaika. 

Mbuzi akasema " Endelea mwanangu, sasa 
soma ubeti wa pih, maneno ya kwanza ndiyo 
' Nihona, njiani.' " Ehsi hakuthubutu kuka- 
taa. Akasoma hivi: 

Nihona njiani, nihpongoja, 
Chui na bundi wakila pamoja; 
Mnyama 'kaguna, akala kwa pupa 
Nyama, mchuzi na hata mifupa. 
'Kamwambia Ndege 'Umekula zamani, 
Posho lako mwenzangu ndilo sahani; 
Na kwa ukarimu nakupa kijiko; 
Mah yangu ni kisu na uma. Na mwiko 
Wangu si bundi. Kwa ghafula ah- 
Mla Bundi na chumvi kwa meno makah. 

Mbuzi akasema " Basi ! Sisi hatuwezi ku- 
fahamu hata neno moja, eleza." Ehsi aka- 
jibu " Siwezi kueleza." Mbuzi akaondoka aka- 
sema " Vema ! Tucheze tena. Au labda uta- 
penda kusikia wimbo wa Kasa Mhaji ?" Kasa 
akacheka akafikiri ya kuwa ahkuwa amesi- 
£wa, Mbuzi akasema " Uimbe wimbo wa NGOMA YA KAMBA 99 

chakula Kaka." Kasa Mliaji akavuta pumzi 
akaimba : 

Key C. 
{| d :r 1 d :n | n :- | r :d | r :d | :- | d :r 1 d :n | n :- | r :d | 
Twen-de mwe-nza-ngu, s - a-sa saa Tu-le cha-ku-la, chaa 

{ I r :d I :- | pi :f | n :s | s :f | n :f | n :- | : | s :t, | t, :t, | d :r | r :d | 
ku-faa, I-ko na-fa-si na . . wa-saa Tu-le cha-ku-u-la cha ku- 

{ I d :- I - :- I d :n .Pi I d :n .n | s .d :r | s :f | n :r | d : || 
faa. Cha ku-faa, cha ku-faa, Tu-le cha-ku-la cha ku-faa. 

Twende mwenzangu, sasa saa 
Tule chakula, njoo kukaa, 
Iko naf asi na wasaa 
Kula chakula cha kufaa. 
Cha kufaa, cha kufaa. 
Kula chakula cha kufaa. 

Sisi mwenzangu mashujaa, 
Nasi twaona njaa njaa. 
Tusitandike kitambaa, 
Tule chakula cha kufaa 
Chakula kizuri cha kufaa 
Tule chakula cha kufaa. 

Mbuzi akapaza sauti akasema " Tuitikie !" 
Wote wakawa katika kuitikia wakiimba " Tule 
chakula cha kufaa." waHposikia sauti mbali 
kidogo, wakanyamaza wakasikiliza, halafu wa- 
kamwona Askari mmoja ambaye alikuwa aki- 100 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

zitangaza amri za Mfalme Mzunguwanne. Ta- 
ngazo lenyewe lilikuwa hili: " Njooni Wote ! 
HuKUMU Kuu Ni Tayari. Njooni. Njoo- 
Ni." Mbuzi akamshika EUsi mkono akasema 
"Twende." 

Elisi na Mbuzi wakaenda pamoja kwa ha- 
raka; lakini Kasa MHaji hakuondoka, akaende- 
lea kuimba na kutoa machozi. 

EUsi alimsikia kwa mbali akiimba: 

Chakula kizuri cha kufaa 
Tule chakula cha kufaa. 
"-^^^^^^WM^^ SURA XI 

MWIZI WA MAANDAZr 

Walipokuwa wamefika Bomani Elisi na Mbu- 
zi walimwona Mfalme Mzunguwanne wa Kopa, 
na Malkia Mzunguwapili wa Kopa, walikuwa 
wamekaa penye viti vyao vya enzi, na mbele 
yao mkutano mkubwa wa viumbe. 

Mjanja Mzunguwatatu wa Kopa alikuwa 
amefung\^a kwa minyororo, naye alikuwa ame- 
simama kati ya Askari wawili. 

Sungura Mweupe alikuwa akisimama, penye 
kiti cha enzi cha Mfalme, alikuwa akishika 
tarumbeta na cheti. 

101 102 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU Katikati kabisa ya Boma palikuwa na meza, 
na juu ya meza ilikuwa sahani kubwa yenye 
maandazi. 

Mfalme alikuwa mwamuzi, na alikuwa ame- 
vaa kofia ya ujaji na juu ya kofia ile, amevaa 
taji. Penye baraza ndogo wakakaa viumbe 
thenashara, ambao waHkuwa wakiandika ka- 

tika vibao vyao kwa 
bidii. Elisi akamwu- 
liza Mbuzi akasema 
" Wanaandika nini ?" 
Mbuzi akajibu " Wa- 
naandika majini yao 
wasiyasahau." Elisi 
akasema " W a p u- 
mbafu!" 

Sungura Mweupe 

akapiga sana taru- 

mbeta, akatangaza 

kwa sauti kuu aka- 

s e m a " Ny amazeni 

watu wote." 

Mf alme akavaa miwani akatazamatazama, apa- 

te kuona ya kwamba wote waUkuwa wametulia. 

EHsi akavitazama vibao vya viumbe the- 

nashara. Akacheka sana hawakujua hata 

mmoja kuandika sawasawa. Elisi akasema 

kimoyomoyo " Lakini hawa si binadamu. Nao- 

na mjusi mmoja, panya mmoja, chura mmoja, 

bata, kuku, kenge, komba na wengineo, si aja- 
MWIZI WA MAANDAZI 103 

bu kubwa ya kuwa hawajui kuandika." Mfa- 
Ime akapaza sauti akasema "Soma mashtaka." 
Sungura Mweupe akapiga tarumbeta mara tatu 
akatangaza mashtaka, akasema " Malkia ali- 
pika maandazi, 

Na yalikuwa mazuri bila shaka, 
Akaja mwizi alfajiri sana, 
Na aliyaondoa kwa haraka." 

Mfalme akamwambia wathenashara " Fiki- 
rini sana." Sungura Mweupe akapiga tena ta- 
rumbeta akasema " Mshahidi wa kwanza si- 
mana." Mshahidi wa kwanza alikuwa Mwu- 
za Kofia. Akasimama, akakaribia kidogo kiti 
cha enzi, nyuma yake wakaja Kobe na Komba. 
Mwuza Kofia ahkuwa akishika kikombe na 
kipanda cha mkate, akawasujudia sana Mfahne 
na Malkia, akasema " Niwieni radhi Bibi na 
Bwana, lakini nilikuwa sijaisha chakula cha 
jioni nilipoitwa nanyi." Mfalme akasema 
" Shauri hili mbaya; kwa sababu gani hujaisha 
kula ? UHanza kula lini ?" Mwuza Kofia 
akamtazama Kobe akasema " TuUanza kula 
chakula cha jioni terehe 14 Machi." Kobe 
akasema " La ! Terehe 15 Machi." Komba 
akajibu " La ! Ilikuwa 16 Machi." Mfalme 
akawaambia wathenashara " Andikeni maneno 
haya." Viumbe wakaandika zile terehe tatu, 
wahazihesabu wakaandika jumla kana kwamba 
zilikuwa shilingi na senti. 104 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU Mfalme akamwambia Mwuza Kofia akasema 
'' Vua kofia yako." Mwuza akajibu " Si kofia 
yangu." Mfalme akapiga uruzi akasema 
' ' Umeiiba ? " Akawaambia wathenashara 
" Andikeni." Mwuza Kofia akaeleza kwa ha- 
raka akasema " Mimi mchuuzi, dukani mwa- 
ngu ziko kofia nyingi sana, lakini si zangu za 
kuvaa, naziuza tu." Kwa ghafula Malkia aka- 
vaa miwani, akamtazama sana Mwuza Kofia. 
Huyo, alipoona kuwa Malkia alikuwa akimta- 
zama alitetemeka kwa hofu. Mfalme akasema 
" Toa ushahidi, wala usiogope ih nisikukate 
kichwa sasa hivi." Mwuza Kofia akazidi kute- 
temeka na kubabaika, na katika kufadliaika 
kwake ahkimegua kikombe badala ya mkate. 

Wakati ule ule EHsi ahona ajabu mwihni 
mwake, baadaye ahfahamu ya kwamba ahku- 
wa akiongeza tena urefu; akawaza kuwa afa- MWlZI WA MAANDAZI 105 

dhali atoke Bomani, lakini halafu aliona ni 
heri azidi kukaa, kama ikiwapo nafasi. Ko- 
mba alikuwa amekaa karibu na Elisi akasema 
" Usinisukume mwanangu, sioni wasaa hata 
wa kuvuta pumzi !" Elisi akajibu kwa unye- 
nyekevu, akasema " Sina budi nikusukume, 
sababu mimi naongezeka urefu." Komba aka- 
sema " Huna ruksa kuongeza urefu hapa." 
Elisi akajibu " Wewe unaongezeka pia." Ko- 
mba akaondoka akasema " Najua sana, lakini 
mimi nakua kwa pole pole, si kama wewe, kwa 
haraka sana." Komba akamwacha Ehsi aka- 
kaa mahali pengine. Komba na EKsi walipo- 
kuwa wakisemezana, Malkia alikuwa anazidi 
kumtazama Mwuza Kofia; akamwambia Askari 
mmoja akasema " Niletee karatasi yenye ma- 
jina ya waimbaji wa machezo ya terehe 13 
Machi." Aliposikia maneno haya M^Tiza Ko- 
fia akazidi mno kutetemeka mpaka viatu vyake 
vikamtoka miguuni; Mfalme akasema " Toa 
ushahidi mara moja." Mwuza Kofia akajibu 
akasema " Uwe na rehema, mimi maskini, sina 
akili." Mfalme akapiga kofi akasema " Nenda 
zako. Mjinga." Mwuza Kofia akajibu " Nipe 
ruksa kwanza niishe kula chakula cha jioni." 
Alipokuwa akisema Malkia alikuwa akilitafuta 
jina lake katika majina ya waimbaji. Mfalme 
akasema kwa upole "Mwuza Kofia we, nenda 
zako." Malkia akapaza sauti akasema " Mka- 
te kichwa huko nje. Huyu ndiye ahye- 106 ELISI KATIKA KCHI YA AJABU 

mwua Nafasi zamani kidogo." Mwuza Kofia 
hakukaa kuyasikia maneno haya, akaviacha 
viatu Bomani, akakimbia kwa haraka ka- 
ma umeme hata hakuweza kukamatwa na 
Askari. Mfalme akaondoka akasema kwa sauti 
kuu akinena " Mwita mshahidi wa pili." 
Mshahidi wa pili ahkuwa Mpishi wa Mama 
Mkubwa; alikuwa amechukua chupa ya pili 
pih. Mfalme akamwambia " Toa ushahidi 
wako." Mpishi akajibu " Sitaki." Sungura 
Mweupe akamwambia Mfalme akasema " La- 
zima umshurutishe aseme." Mfalme akapiga 
chafya akafunga mikono akamtazama sana 
Mpishi akasema " Maandazi yaHtengenezwa 
kwa kitu gani ?" Mpishi akajibu " YaHtenge- 
nezwa kwa piH piH." Komba akaondoka aka- 
sema kwa sauti nyembamba " YaHtengenezwa 
kwa asaH !" Malkia akanong'ona akasema 
*' Akatwe kichwa yule Komba." Wote waka- 
simama wakapiga mbio huko na huko, waka- 
jaribu kumkamata Komba; iHkuwa ghasia ka- 
bisa Bomani, lakini watu waHshindwa. Komba 
akapanda darini. Watu wote waHkuwa wame- 
choka, wakapumzika, na kumbe Mpishi naye 
aHkuwa ametoroka ! Mfalme akasema " Hai- 
dhuru, mwite mshahidi mwingine." Akamwa- 
mbia Malkia kwa sauti ndogo akasema •" Tafa- 
dhaH mpenzi, wewe umwuHze mshahidi huyu, 
kichwa kinaniuma." 

EHsi akamtazama Sungura Mweupe, aHye- MWIZI WA MAANDAZI 107 

kuwa akitafuta jina la mshahidi wa tatu katika 
cheti chake. Sungura Mweupe akasimama wi- 
ma, akapiga sana tarumbeta mara tatu, aka- 
sema kwa sauti kuu: 

" Elisi." 
V!i^\V> SURA XII 

USHAHIDI WA ELISI 

Elisi alishtuka sana kusikia jina lake likita- 
jwa; lakini akasimama mara akaitikia " Sa !" 
Kwa sababu ya urefu wake mkubwa akaangu- 
sha baraza ya wathenashara. Akafadhaika 
sana akasema " Niwieni radhi, niwieni ra- 

108 USHAHIDI WA ELISI 109 

dhi !" Akawasaidia wanyama kutengeneza tena 
meza, na kutafuta vibao vyao na kalamu 
zao. 

Wote walipokuwa tayari Mfalme alimwuliza 
Elisi akasema " Unajua niai katika mambo 
haya ?" Elisi akajibu " Sijui kitu." Mfalme 
akawaambia wathenashara akasema " Andi- 
keni ' Hajui kitu.' " Mfalme akamtazama EHsi 
akafadhaika akatoa kitabu kidogo katika mfu- 
ko akasoma, akakirudisha mfukoni, akamta- 
zama tena EHsi akasema " Sikilizeni. Amri 
ya arobaini na nne ya Boma hili ndiyo : ' Wote 
wenye urefu kupita mnazi wafukuzwe Bomani.' " 
Wote wakamtazama Ehsi. Eajana akasema 
" Urefu wangu si wa kupita mnazi." Mfalme 
akajibu '' Ni kupita miaazi miwih." EHsi aka- 
sema " Sitaondoka. Hii si amri ya tangu za- 
mani, umeizua sasa hivi katika haja yako ?" 
Mfahne akajibu akasema " Ni amri ya kale 
kupita zote kitabuni." Ehsi akacheka akasema 
" Ikiwa hivyo, basi sharti iwe ya kwanza, 
nawe uhkuwa ukitazama katika ukarasa wa 
mwisho kitabuni." Mfahne hakujibu, akafa- 
dhaika kabisa, akaondoka katika kiti chake cha 
enzi, akapaza sauti akasema " Wakubwa wa 
Baraza wakate shauri." Malkia Mzunguwapih 
akaondoka akamwelekeza kwa kidole Mjanja, 
ahyekuwa mfungwa, akasema " Kwanza mkate 
kichwa huyu." Ehsi akasema " Hapana Ma- 
ma, Kwanza hukumu, halafu kuuawa, ikiwa 110 ELISI KATIKA NCHI YA AJABU 

amestahili." Malkia akanong'ona akasema 
*' Nyamaza we." Elisi akajibu " Siwezi ku- 
nyamaza." Malkia akasema Kwa sauti kali 
akanena " Mkate kichwa Ehsi !" USHAHIDI WA ELISI 111 

Elisi akawatazama Askari akatabasamu kwa- 
ni hakutokea hata mtu mmoja wa kutimiza 
amri za Malkia. 

Elisi akajitazama, akaona kuwa urefu wake 
ulikuwa kama zamani, kama mtoto wa nchi 
wa Afrika. Akawatazama wenyeji wa Nchi 
wa Ajabu akasema: " Siwaogope . . . 

NiNYi Nyote Karata tu. 
!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! 
Kwa maneno haya karata zote zikaruka he- 
wani zikampiga usoni Elisi. 

Yeye akafumbua macho, akapiga yowe. . . . 

Akaamka. 
!!!!!!! 

Alipokuwa macho akajiona, na kumbe aliku- 
wa amelala chini ya mwembe ! Dada yake 
alikuwa amekaa karibu akimfukuzia mdudu 
aliyekuwa ametambaa usoni, akasema " Amka 
Elisi mwanangu, umelala sana." EHsi akao- 
ndoka akajinyosha akasema " Kweh ! Tena 
nimeota sana." AkamsimuUa Dada habari za 
ndoto yake. 

Alipokwisha kuhadithia ndugu yake aka- 
mwambia " Twende mwanangu, Mama ana- 
twanga, chakula cha jioni ni karibu tayari, na 
Dina anakuhha." 

MWISHO. PRINTED IN GREAT BRITAIN BY 
FLETCHER AND SON LTD NORWICH